KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 1, 2014

Pamoja na kustaafu kucheza soka David Beckham adhihirisha mapenzi yake katika mchezo wa Baseball

 David akiwa na Brooklyn, Romeo na Cruz akiangalia mchezo wa Baseball wakiishabikia Los Angeles Dodgers Alhamisi iliyopita

Anaweza kweli akawa amejiuzulu kucheza soka la kulipwa mwaka uliopita, lakini michezo kwake ni kama imechukua sehemu kubwa ndani ya moyo na maisha ya  David Beckham.
Kiungo huyo wa zamani wa LA Galaxy ametumia sehemu kubwa kuwachukua watoto wake Brooklyn, 15, Romeo, 11, na Cruz, 9 kwenda kuangalia mchezo wa Baseball ambao timu yake ya Los Angeles Dodgers ilikuwa ikicheza huko Dodger Stadium jijini Los Angelos Alhamisi usiku.
Watoto hao wa kiume wa Beckham wameonekana kufurahia mchezo huo wakiwa na baba yao wakati timu yao ya nyumbani ilipoichapa Atlanta Braves 2-1.
Like father, like son: David shared a laugh with nine-year-old son Cruz
Like father, like son: David akifurahi na mtoto Cruz mwenye umri wa miaka tisa

Beckham alikuwa amevalia kapelo ya Dodgers na alipigwa picha akiwa na watoto wake wakizungumza mchezo huo.

Wakati huohuo mama wa watoto hao wanne Victoria alikuwa amesalia nyumbani akiendelea na malezi ya matoto pacha wa kike wenye umri wa miaka miwili Harper.
Daddy duties: Brooklyn and Cruz engaged David in an in-depth discussion about the game
Majukumu ya baba: Hapa Brooklyn na huku Cruz wakipiga stori kuhusu game

Loyal supporters: Fans seemed nonplussed to see the famous family as they are regulars at Dodgers games

Beckham amekuwa akijishughulisha na mambo ya maonyesho ya mavazi( underwear collections for H&M) tangu alipoachana na soka Mei 2013.

Katika kipindi chake cha miaka 20 ya uchezaji soka, mbali ya kuichezea na kuwa nahodha wa timu ya taifa ya England, amechezea vilabu kadhaa kama vile Manchester United, Real Madrid, Milan, Los Angeles Galaxy na Paris Saint-Germain.
Family time: The sports star has been making the most of spending time with his sons this summer