Davis Mosha mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga. |
Msemaji mpya wa Yanga Baraka Kizuguto. |
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga hii leo imewatangaza watendaji wake wapya ikiwa ni pamoja na kumteua aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti huko nyuma Davis Mosha kuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano.
Watendaji wapya waliotangazwa hii leo ni pamoja na meneja mpya Shabani Katwila ambaye anachukua nafasi ya Hafidhi wakati ambapo Baraka kaziguto anachukua nafasi ya Luis Sendeu aliyemaliza mkataba wake.
Kamati ya mashindano chini ya Mosha itakuwa na wajumbe Muzamil Katunzi pamoja na Beda Tindwa ambao bila shaka watakuwa na jukumu la kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Akiwatambulisha mbele ya waandishi wa habari Katibu mkuu wa Yanga Laurence Mwalusako amesema Yanga Afrika wanaamini watendaji hao pamoja na viongozi walitangazwa hii leo watawasaidi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akiongea na waandishi wa habari Shabani Katwila amesema yeye anajimini kuwa anaweza kufanya kazi yake kwa kuwa alishawahi kuwa mchezaji huko nyuma na kwamba umri wake licha ya kuwa ni mkubwa lakini anaamini atafanya kazi zake vizuri kwa kuwa hata Ferguson meneja wa Manchester United ana umri mkubwa lakini anafanya kazi zake vizuri.
Naye msemaji mpya Baraka kaziguto amesema anaamini atafanya kazi zake vizuri kwa kuwa ana elimu ya mambo ya uandishi wa habari na pia anajua vizuri mambo ya kompyuta hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wanahabari hao katika kutimiza majukumu yake.
Katika hatua nyingine,
Mwalusako amesema mkutano mkuu wa Yanga utafanyika desemba 16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment