Jumla ya vilabu 12 kati ya vilabu 14 vinavyoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara hii leo vitakuwa dimbani kumaliza michezo yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya soka Tanzania bara michezo ambayo itakuwa ikipigwa katika viwanja sita tofauti.
wakati michezo hiyo ikitarajiwa kupigwa jioni ya leo, mabingwa wa soka Afrika mashariki na kati Yanga wanaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo wakiwa na alama 26 wakifuatiwa na Azama fc wenye alama 24 huku Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hilo baada ya kukusanya jumla ya alama 23.
Wao Azam leo watakuwa katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga wakiwa ni wageni wa Mgambo JKT ambao hali kwao haikuwa nzuri mpaka kufikia michezo kwani baada ya michezo 12 wameweza kujikusanyia alama 11 tu.
Endapo Azam atashinda katika mchezo wa leo watakuwa wamefikisha jumla ya alama 27 na hivyo kuongoza ligi hiyo huku yakisubiriwa matokeo ya mchezo wa mwisho wa kesho wa Yanga dhidi ya Coast kule Tanga
Endapo Azam atashinda katika mchezo wa leo watakuwa wamefikisha jumla ya alama 27 na hivyo kuongoza ligi hiyo huku yakisubiriwa matokeo ya mchezo wa mwisho wa kesho wa Yanga dhidi ya Coast kule Tanga
Simba hii leo watakuwa wenyeji wa Toto Afrika ya Mwanza mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba watakuwa wakihitaji ushindi kwa namna yoyote ile ambapo mbali na kutaka kurejesha imani kwa mashabiki wake.
Lakini pia watakuwa wakihitaji ushindi ili kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi wakiwa na alama 26 sawa na Yanga japo kwa siku moja wanaweza kuongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kunga na kufungwa kabla ya watani zao hao hawajashuka dimbani hiyo hiyo kesho katika dimba la Mkwakwani kucheza dhidi ya wenyeji Coast union na endapo Yanga atafungwa basi Simba watakuwa wamemalizia mzunguko huu wakiwa kinara.
Kumbuka Coast ni timu ngumu ambayo mpaka sasa baada ya michezo 12 ya ligi hiyo imefanikiwa kukusanya alama 22 ambazo zimewaweka katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.
Kama hiyo haitoshi JKT Oljoro wao watakuwa katika dimba la sheikh Amri Abeid Kaluta kucheza dhidi ya timu ngumu ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar watakuwa katika uwanja wao wa Kaitaba kuwakaribisha watoto wa afande Mahita Polisi ya Morogoro.
Kwa upande wao Afrikan Lyon wao watakuwa katika dimba la Azam Complex kule Chamazi kumalizia mzunguko wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo katika mzunguko huu wa kwanza walikuwa ni sumu kwa vigogo vya soka Simba na Yanga baaada ya kuwachapa kila mmoja kwa wakati wake katika michezo iliyofanyika katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.
Mpaka kufikia hapo msimamo wa ligi umesimama kama unavyoonekana hapo chini
Msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzani Bara msimu wa 2012/2013 ni kama hivi
Rank | Teams | Played | Wins | Draw | Lost | GD | Points |
---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 12 | 8 | 2 | 2 | 13 | 26 |
2 | Azam FC | 12 | 7 | 3 | 2 | 7 | 24 |
3 | Simba SC | 12 | 6 | 5 | 1 | 10 | 23 |
4 | Coastal Union | 12 | 6 | 4 | 2 | 4 | 22 |
5 | Kagera Sugar | 12 | 5 | 5 | 2 | 5 | 20 |
6 | Mtibwa Sugar | 12 | 5 | 4 | 3 | 4 | 19 |
7 | Ruvu Shooting | 11 | 4 | 2 | 5 | -1 | 14 |
8 | JKT Oljoro | 12 | 3 | 5 | 4 | -2 | 14 |
9 | JKT Ruvu | 12 | 4 | 2 | 6 | -7 | 14 |
10 | Prisons FC | 10 | 3 | 4 | 3 | -1 | 13 |
11 | Mgambo Shooting | 11 | 3 | 2 | 6 | -5 | 11 |
12 | Toto African | 12 | 1 | 6 | 5 | -6 | 9 |
13 | African Lyon | 12 | 2 | 3 | 7 | -9 | 9 |
14 | Police M | 12 | 0 | 3 | 9 | -12 | 3 |
Hakika mzunguko huu utakuwa unamalizika huku kukijitokeza changamoto mbalimbali ambazo kila mwaka zimekuwa zikijitokeza ama kwa kujirudia au kujitokeza changamoto mpya ambazo bila shaka zitahitaji dawa yake. | ||||||||||||
Itakuwa n i mapema mno kuzungumza chochote juu ya changamoto hizo kwa leo isipokuwa tusubiri mchezo wa kesho wa kufunga kabisa ukurasa wa mzunguko wa kwanza ili tuweze kuziangalia katika kona mbalimbali. | ||||||||||||
kwasasa zipo mbili ambazo zimejitokeza waziwazi ikiwa pamoja na kuingia na kutoka kwa makocha wakigeni katika vilabu viwili vikubwa hapa nchini kutoka na ama kupoteza imani kwa viongozi wa vilabu hivyo au woga wa viongozi katika kusaka matokeo mazuri na hata kuogopa lawama za wapenzi na mashabiki wa vilabu hivyo. | ||||||||||||
Inawezekana pia ikawa ni kutokueleweka vizuri kwa majumu ya kila mmoja na hata muingiliano wa kimajukumu na kukwepa ukweli juu ya uweledi wa mtu na kutokutimiza wajibu. | ||||||||||||
kwasasa tuishie hapo. | ||||||||||||
Kwa vilabu ambavyo vinamaliza mzunguko wa kwanza leo navitakia kila kheri wamalize kwa ushindi na mchezo safi unaoridhisha watazamaji ambao ndio wadau wenu wakubwa. | ||||||||||||
lakini pia mjifunze kutokana na makosa yaliyochomoza katika mzunguko huu. | ||||||||||||
Suala la tuhuma za rushwa tunazungumza siku nyingine kwani liko katika vyombo vya sheria. | ||||||||||||
No comments:
Post a Comment