Sir Alex
Ferguson amesisitiza kuwa Manchester United haimtegemei sana Robin van Persie
ambaye kwasasa yuko katika kizuri.
Van Persie aliyejiunga
na United akitokea Arsenal majira ya kiangazi alianza maisha yake mapya katika
viunga vya Old Trafford kwa kung’ara
baada ya kufunga mabao 11 katika jumla ya michezo 14.
Mholanzi huyo
ambaye alianzia benchi katika mchezo dhidi ya Braga mchezo wa vilabu bingwa
ulaya alidhihirisha ubora wake baada ya kuingizwa dimbani kwa kufunga goli la
pili zuri na hivyo maswali kuanza kuibuka juu ya uwezo wa United kucheza bila
ya yeye.
Vijana wa
mzee Ferguson sasa wamekuwa wafunga magoli katika kila mchezo ambapo
mshambuliaji huyo gumzo nchini England na duniani kwa ujumla akiwa ni miongoni
mwa wafumania nyavu wa juu katika ligi ya England na ligi ya mabingwa ulaya.
"sidhani
kama ni tatizo kumtegemea Robin, mwaka jana tulipoteza taji kwa tofauti ya bao
la kufunga na kufungwa . sitaki kupoteza tena taji kwa tofauti ya mabao ya
kufunga na kufungwa"
Van Persie tangu
ajiunge na United amekuwa akiwakumbusha mashabiki wa United enzi za Ruud van
Nistelrooy jambo ambalo hata hivyol Ferguson hapindezwi nalo.
"Robin ni
mchezaji tofauti na van Nistelrooy,"
"Ruud alikuwa
ni mshambuliaji wa ndani ya kisanduku cha hatari lakini . Robin yuko katika utofauti
katika kuelewa mchezo"
"hatukudhani
kama tungempata. Kulikuwa na dhana kuwa huenda Arsenal ingefanikiwa kumbakisha
Emirate"
Lakini alipoamua kundoka tulipata nguvu mpya kwa kwa kweli ni miongoni
mwa wachezaji bora katika biashara ya soka."
Leo United
watakuwa dimbani dhidi ya Aston Villa.
Chelsea hawako tayari kumuachia Cole
aondoke.
Klabu ya Chelsea
imesema kuwa haiko tayari kumuachia mlinzi wake wa pembeni Ashley Cole aondoke na kujiunga na Paris
Saint-Germain au hata klabu nyingine kubwa barani Ulaya mnamo mwezi Januari.
Mabingwa hao
wa soka wa vilabu barani Ulaya wamethibitisha juu ya kuendelea kuwepo kwa
mazungumzo baina yao na mwakilishi wa Cole na kwamba huenda wakafikia tamati
kabla ya sikukuu ya Christmas katika kujaribu kumzuia mlinzi huyo na huenda
akasaini mkataba mpya.
Meneja wa
klabu hiyo Roberto Di Matteo na viongozi wengine waandamizi wa klabu hiyo
wamekuwa wakimtaka mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kuachana na mpango
wake wa kuwaacha wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30 na kumuongezea Cole mwaka
mmoja baada ya mkataba wake kumalizika.
No comments:
Post a Comment