Beki wa Toto African Elly Hamad akimdhibiti Haruna Chanongo wa Simba kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa taifa |
Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akiwa amedhibitiwa na kiungo wa Toto African Peter Mutabuzi kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa Taifa |
Kiungo wa Simba Amri Kiemba akimtoka beki wa Toto African kwenye mchezo uliochezwa taifa |
Wachezaji wa Toto wakimpongeza mfungaji wa bao lao baada ya mchezo waliocheza leo kwenye uwanja wa taifa na Simba baada ya mchezo kumalizika. |
TIMU ya Simba leo imemaliza mzunguko wa kwanza kwa kufungwa na Toto
African bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Bao pekee la Toto lilifungwa na Mussa Said Kimbu dakika ya 73.
Kimbu alifunga bao hilo baada ya kupiga direct free kick baada ya kutokea faulo na mpira huo kuwapita walinzi wa Simba na kipa wao Wilbert Mweta na kutinga wavuni.
Michezo mingine ya ligi iliyochezwa leo ni pamoja na Azam dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo wanalambalamba hao Azam wamefungwa 2-1.

Kwa matokeo haya, Yanga inazidi kukaa kileleni kwa pointi zake 26 na kesho itamaliza mechi yake ya mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.
Simba SC: Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Emanuel Okwi.
Toto African; Erick Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo, Evarist Maganga, Peter Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita, Kheri Mohamed, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Sai.
(Chanzo Lenzi ya michezo)
No comments:
Post a Comment