KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 11, 2012

JE NI KWELI YANGA INAKWENDA KUMALIZA KAZI MKWAKWANI TANGA JIONI YA LEO. JE COASTAL UNION ITAKAMATA NAFASI YA PILI.

Wapenzi na wanachama wa Yanga wameendelea kutamba kuwa timu yao itaingia katika dimba la Mkwakwani jioni hii kwa lengo la kupata ushindi na kumalizia kazi ya kufunga duru la kwanza kwa ushindi mkubwa dhidi ya Coastal Union ya huko.

Tayari huko mkoani tanga kwenyewe homa imepanda kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili huku kila upende ukitamba kufanya vizuri zaidi na kupata matokeo mazuri pia.

Yanga yenye alama 26 endapo itashinda mchezo wa jioni hii itakuwa imefikisha alama 29 ambazo zitakuwa ni zaidi ya alama 5 kwa Azam ambayo tayari amemaliza duru la kwanza kwa kufungwa na Mgambo JKT bao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja ambao utatumika kumalizia duru wa Mkwawani.

Coastal Union imeapa kumkwamisha Yanga hii leo na kwamba uwezo huo wanao ikizangatiwa uwezo wa wachezaji mmoja mmoja lakini pia nidhamu ya kimchezo ya wachezaji wake hiyo ikiwa ni kauli ya viongozi wa Coastal kama walivyonukuliwa na radio moja hapa nchini jana.

 Mashabiki wengi wa Yanga kutoka katika jiji la Dar es Salaam, Pwani, Moshi na hata Morogoro wako jijini Tanga ama wanakaribia kuingia katika jiji hilo kushuhudia mchezo huo.

Kama ilivyokuwa kwa Simba ilivyopata tabu kwa Toto Afrika basi na Yanga ndivyo inavyokuwa inapokutana na Coastal licha ya mwaka jana Yanga kuvuna mabao 5-0 mwezi septemba na kuonekana ilikuwa kazi rahisi. 

Kumbuka endapo Coastal itashinda itafikisha alama 25 na hivyo kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
 
  Coastal Union wanahitaji ushindi ili kuziacha Azam na Simba na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Coastal wanajua wazi kuwa yanga imepania mchezo wa leo na hivyo imejipanga vilivyo kuhakikisha wanaidhiri Yanga na kukalia nafasi hiyo ya pili ambayo kama watashindwa kufanya hivyo basi huenda wasishike tena nafasi hiyo msimu huu kutokana na Simba na Azam watakavyo rudi katika duru la pili. 

Tambo na majigambo katika soka mwisho wake ni baada ya dakika 90 mchezo hivyo basi tusubiri tuone itakuwaje. 
 

No comments:

Post a Comment