Sehemu ya mashabiki wa England katika mchezo dhidi ya San Marino. |
Mtandao wa kupambana na vitendo vya kibaguzi wa rangi katika
soka barani Ulaya (FARE), umeishitaki England kunako shirikisho la soka duniani
FIFA kufuatia mashabiki wa nchi hiyo kumshambulia kwa maneno ya kibaguzi wa
rangi Rio Ferdinand na ndugu yake Anton siku ya Ijumaa, wakati wa mchezo wa
kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino.
FARE wameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
wa Twitter kuwa wametuma taarifa hiyo FIFA kuliarifu shirikisho hilo kuhusu kujitokeza
kwa mambo ya kibaguzi katika mchezo huo, ambao England ilichomoza na ushindi
mnene wa mabao 8-0 dhidi ya San Marino.
Mlinzi wa kati wa Manchester United Rio Ferdinand mwenye
umri wa miaka 34, aliitwa na meneja wa England Roy Hodgson kwa ajii ya michezo
miwili ya kufuzu dhidi ya San Marino na Montenegro lakini mlinzi huyo
aliondolewa kikosini.
Mlinzi huyo ambaye haja itumikia timu aya taifa tangu mwaka 2011,
aliondolewa kikosini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa fiti lakini
badala yake akaelekea Qatar kufanya kazi uchambuzi katika televisheni ya
Aljazeera.
Hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyopelekea Rio na Anton Ferdinand
kukumbwa na kadhia hiyo ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa England.
Mkurugenzi mtendaji wa FARE Piara Powar amesema kuwa licha
ya kwamba hawakuwa na waangalizi katika mchezo huo lakini wamekusanya ushahidi
wa kutosha ikiwa ni pamoja na maoni ya vyombo vya habari na kuwasilisha FIFA.
Bado chama cha soka nchini England hakijatoa maoni yoyote
kuhusiana na tukio hilo.
Rio Ferdinand picha ya juu na Anton Ferdinand picha ya chini kushoto.
No comments:
Post a Comment