KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, March 29, 2013

BONDIA ROBERT GUERRERO AKUTWA NA SILAHA UWANJA WA NDEGE JOHN F KENNEDY, NINI KITAMSIBU BAADAYE..........................

 Floyd Mayweather
Bondia Robert Guerrero hapo jana alikamatwa na kutiwa ndani katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy jijini New York kufuatia jaribio lake la kuindia ndani ya ndege akiwa na bastola.

Bondia huyo anayepigana uzito wa welterweight, ambaye anatarajia kucheza pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather Jr. jijini Las Vegas Mei 4, aliripotiwa kuwa alikuwa na bastola aina ya a .40-caliber Smith & Wesson na magazini tatu wakati akielekea California.

Guerrero ambaye alikuwa jijini New York kwa ajili ya kulitangaza pambano lake linalo kuja atalazimika kufunguliwa mashitaka  kwa kosa la jinai kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Inadhaniwa kuwa makosa hayo aliyokutwa nayo hayata athiri hadhi ya nyota huyo wa masumbwi zaidi ya kwenda jela miaka minne endapo atakutwa na hatia.

Robert Guerrero
Floyd Mayweather

Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi  Guerrero, ambaye anacho kibali cha kumiliki na kutembea na silaha katika jiji la California lakini hajapewa kibali cha haruhusiwa kutembea nayo kila mahala na inaarifiwa pia aliwahi kuwa silaha alipowasili New York alipokuwa akitoka Virginia. 

No comments:

Post a Comment