Katika picha: Samed Yesil, Jordan Ibe, Kristoffer Peterson, Craig Roddan, Ryan McLaughlin na Jack Dunn. |
Wachezaji vijana wa Liverpool wameonyesha upendo wao na kuguswa na watoto walioko mahospitalini katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Pasaka.
Kama inavyofanywa na watu mbalimbali nyakati kama hizi za sikukuu ya Pasaka na wao pia wamewatembelea watoto na kuwapa zawadi katika hospitali iliyoko karibu na klabu yao ya Liverpool.
Jumla ya vijana wa klabu hiyo kumi na moja kutoka katika kituo cha kukuzia vipaji cha klabu hiyo, wametembelea hospitali ya Alder Hey jana na kuzungumza na watoto ambapo wataendelea kuwepo hospitalini hapo kipindi chote za sikukuu ya Pasaka.
Mlinzi Conor Coady mwenye umri wa miaka 20, ambaye alikuwepo katika kikosi cha kwanza cha Liverpool katika mchezo dhidi ya Anzhi Makhachkala katika michuano ya Ulaya 'Europa League' naye alikuwa ni miongoni mwa hao waliofanya ziara hiyo.
Amekaririwa akisema kinda huyo akisema
‘Kufanya ziara kwa watoto hao ilikuwa jambo kubwa'.
Ameendelea kwa kusema,
‘Nina wadogo zangu nyumbani kwa hiyo najua nini maana ya watoto hawa kupata ujio wetu hususani kwa kuwapa faraja katika kipindi hiki.’
Wachezaji hao waligawanyika katika makundi ili kutoa nafasi ya kuzungumza watoto wengi zaidi pamoja na familia zao.
Coady aliuungana na kundi lililokuwa likitoa zawadi ya Chocolate akiwa na wachezaji wengine Lloyd Jones, Jordan Ibe, Ryan McLaughlin, Jack Dunn, na Brad Smith.
Pia alikuwepo Samed Yesil, ambaye mpaka sasa ameshaichezea ligi ndogo ya Capital One michezo miwili kama ilivyokuwa Kristoffer Peterson, Danny Ward, Adam Morgan na Craig Roddan.
Alder Hey Children’s NHS
Foundation Trust ni moja kati ya vituo vya afya vinavyokusanya watoto wengi barani Ulaya ambapo watoto zaidi ya laki mbili hupatiwa huduma kila mwaka.
No comments:
Post a Comment