Na Ezekiel Kamwaga.
Kikosi cha Simba leo kimefanya
mazoezi yake ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya mechi ya kesho
dhidi ya TOTO African ya hapa Mwanza.
Hali ya wachezaji kwa ujumla ni
nzuri na mchezaji pekee aliye kambini ambaye ana hatihati ya kucheza kesho ni
Haruni Chanongo, aliyeumia katika mechi iliyopita dhidi ya KAGERA SUGAR.
Amri Kiemba ambaye hakucheza mechi
ya Kagera anarejea uwanjani baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake kadi tatuza
njano.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig,
amesema pamoja na kupoteza mechi ya Kagera, bado ana imani na vijana wake.
No comments:
Post a Comment