Nahodha wa Fulham Brede Hangeland aongeza
mkataba.
Nahodha wa
wa timu ya Fulham Brede Hangeland ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kusalia
katika viunga vya Craven Cottage mpaka mwaka 2015.
Mlinzi huyo
raia wa Norway makataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu
huu ambapo sasa ameamua kusali hapo kwa miaka mingine miwili
Hangeland
mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na Fulham akitokea FC Copenhagen mwezi January
2008 kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 2.5, na ameitumikia klabu hiyo ya
London ya magharibi kwa zaidi ya michezo mia mbili.
Amekaririwa akisema kuwa amekuwa ni mwenye
furaha katika kipindi chote alichokuwepo ndani ya klabu hiyo.
Bixente Lizarazu amzodoa David Beckham.
Nyota wa
zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Bixente
Lizarazu anadhani kuwa kuwa kiungo wa Paris Saint-Germain David Beckham alikosa
uweledi lipofanya ziara ya kuitembelea china siku chache tu kabla ya mchezo wa
kwanza wa robo fainali dhidi ya Barcelona.
Beckham alizuru
mashariki ya kati wakati wa mapumziko ya michezo ya kimataifa akiwa kama balozi
wa China, ambapo Lizarazu anadhani kiungo huyo wa zamani wa Manchester United alipaswa
kuwa katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Barca.
Akiongea na
TF1, Lizarazu amesema katika hilo hawezi kumuunga mkono Beckham kwa kufanya
ziara siku kumi kabla ya mchezo muhimu wa msimu, na kwamba jambo hilo halikuwa
sahihi.
Beckham ameitumia
PSG jumla ya michezo mitano tu, tangu ajiunge nayo katika msimu wa usajili wa dirisha
dogo la mwezi January.
YOHAN CABAYE ANASEMA MAN CITY HAICHEZI KITIMU KAMA UNITED
Kiungo wa
Newcastle Yohan Cabaye anaamini kuwa Manchester City haichezi kitimu na hiyo
ndiyo sababu kubwa inayoigharimu timu hiyo.
Kikosi cha
meneja Roberto Mancini tayari kinaonekana kupoteza matumaini ya kutetea taji
taji wakati huu ambapo wako nyuma kwa vinara wa ligi hiyo Manchester United
walio mbele yao kwa mwanya wa alama 15 kileleni.
Kuelekea kwenye
mchezo wa Newcastle dhidi ya City, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amedai
kuwa kikosi hicho kimesheheni wachezaji wazuri lakini hakifanyi kazi kwa umoja.
Amenukuliwa
na gazeti la The Sun akisema
"United
ni mashine na kwamba Sir Alex anafanya kazi nzuri katika klabu yake, hata kama
wachezaji wanabadilika kwakuwa anajua ni mchezaji gani atakuwa mzuri katika
timu.
“City
wanawachezaji wazuri lakini bahati mbaya kwao hawachezi kama timu si kama
United"
Cabaye
alikuwa akikabiliana na wakali wa Hispania Xavi, Andres Iniesta na Sergio
Busquets wakati wa mchezo wa kimataifa mchezo ambao Ufaransa walipoteza kwa bao
1-0.
Anatarajiwa
kuchukua sehemu ya kiungo akipambana na Yahya Toure jumamosi pale ambapo
Newcastle watakapokuwa wakipambana dhidi ya Manchester City.
MANCINI AKERWA NA KOMPANY.
Bosi wa
Manchester City Roberto Mancini amemtaka mlinzi wake wa kati Vincent Kompany
kuweka kwanza kipaumbele katika majukumu ya klabu yaike kuliko kuiwakilisha
Belgium.
Mlinzi huyo
mwenye umri wa miaka26 aliitwa na kocha Marc Wilmots kuunda kikosi cha Belgium
kwa ajili ya majukumu ya kimataifa wakati wa mapumziko ya michezo ya kimataifa
huku akikosekana katika timu yake tangu mwezi Januari.
Mchango wa
Kompany uliisaidia Belgium kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na mlinzi huyo
akicheza dakika zote 90 za mchezo mjini Brussels jumanne jambo ambalo
limemuhuzunisha Mancini.
Akinukuliwa
Mancini akiongea na The Manchester Evening akisema
"Wakati
mwingine mchezaji anatakiwa kuelewa kuwa klabu yake ni muhimu zaidi na wala si
semi kuwa timu ya taifa si muhimu na sitawaambia wachezaji wangu kuwa wasicheze
katika mataifa yao"
"hajaichezea
timu yake kwa siku 60 lakini amekwenda kuichezea timu ya taifa ya Belgian,
Sikubaliani na hilo. Wakati mwingine mameneja wa timu za taifa wanapaswa
kuelewa hali ilivyo, hawa wachezaji wanavilabu vyao na wanalipwa mishahara kila
mwezi”.
CHAMA CHA SOKA ENGLAND CHAMTOSA RIO FERDNAND KUBAGULIWA.
Chama cha
nchini England FA kimesema kuwa kimekosa ushahidi wa kwamba mashabiki wa soka
wa chini hiyo waliimba wimbo za kumbagua mlinzi wa Manchester United Rio
Ferdinand na ndugu yake mlinzi wa QPR Anton, wakati wa mchezo baina ya England
maamrufu kama ‘Three Lions' dhidi ya San Marino.
Katika
taarifa iliyotolewa mkurugenzi wa vilabu ndani ya FA Adrian Bevington imesema
kuwa
"Ndani
ya San Marino, tulikuwa na wakuu wa usalama wa FA waliokuwa wakifuatilia
mashabiki wa England ndani ya uwanja , na hiyo inajumuisha rikodi za video
tulizo zifuatilia.”
NIGERIA WATAKA MAREKEBISHO YA RATIBA YA KOMBE LA DUNIA.
Shirikisho
la soka nchini Nigeria NFF limelitaka shirikisho la soka duniani FIFA kurekebisha
ratiba ya michezo ya timu ya taifa ya nchi hiyo ‘Super eagles’ ya mwezi june kwa
lengo la kutaka haki kutendeka huku wakitaka michezo yote ya kundi F ifanyike
siku.
Wiki
iliyopita Fifa ilirekebisha tarehe za michezo ya Super Eagles kufuatia Nigeria
kukabiliwa na michezo mingine ya michuano ya kombe la shirikisho la dunia mwezi
June.
Nigeria
itacheza na Kenya jijini Nairobi Juni 5 kabla ya kusafiri kuifuata Namibia wiko
moja baadaye na pia kuelekea nchini Brazil Brazil kwa ajili ya michezo ya
michuano ya shirikisho
Michuano hiyo
ya shirikisho ambayo itajumuisha mataifa ya Hispania ambao ndio mabingwa wa
dunia pamoja na mataifa bingwa kutoka mabara sita itakuwa ikifanyika nchini
Brazil kuanzia juni 15.
Michezo ya
kufuzu ya hatua ya makundi ndani ya mwezi juni huenda ikafanyika kati ya 5 na 12
ama tarehe zilizokuwa zimepangwa hapo awali juni 8 na 15.
Nigeria wanaongoza
kundi hilo wakiwa wanakabana koo na Malawi wakitofautiana kwa magoli ya kufunga
na kufungwa na wote wakiwa na alama tano baada ya michezo mitatu.
Katibu mkuu
wa NFF Musa Amadu ameelezea sababu ya shirikisho hilo kupeleka ombi lao Fifa
akisema lengo kutafuta haki na kuzuia upangaji wa matokeo.
No comments:
Post a Comment