Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza
kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa
mashabiki wake walihusika katika matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi yao
na Cameroon.
Katika taarifa, FIFA imesema kuwa uchunguzi huo
umeanzishwa baada ya matamshi kutolewa kuwa mashabiki wa Mexico
walionyesha vitendo na matamshi ya kutiliwa shaka.
Aidha duru kutoka FIFA zimeiambia BBC kuwa
wanachunguza ripoti ya matamshi machafu kutoka kwa mashabiki wa timu ya
Brazil pamoja na mabango ya kibaguzi wakati wa mechi kati ya Croatia na
Russia.
Mwaka jana FIFA ilibuni sheria kali ambapo
matamshi ya kibaguzi kutoka kwa shabiki wa soka au mchezaji, yanaweza
kuchochea adhabu kali hata kulazimisha timu husika kucheza mechi bila ya
mashabiki, kunyanganywa alama, kushushwa daraja au hata kufukuzwa
kushiriki mchuano.
No comments:
Post a Comment