TABIA YA KULIMBIKIZA MADENI MADENI KUMEIDHALILISHA TFF. Basi la udhamnini wa NMB lapigwa mnyororo ndani ya viunga vya uwanja wa Karume.
|
Deni la malimbikizo ya makazi ya waamuzi katika hoteli ya SAFINA waliochezesha michuano ya Chalenji mwaka 2011 limepelekea hii leo basi dogo la shirikisho la soka nchini TFF walilopewa na NMB kufungwa mnyororo ndani viunga vya uwanja wa kumbukumbu ya Karume, kufuatia deni hilo kufikia zaidi ya shilingi milioni 51. Pichani juu linaonekana basi dogo aina ya Coaster la udhamini wa NMB likiwa tayari kukokotwa na Breakdown ya kampuni ya Flamingo Auction Mart kufuatia amri ya mahakama ya Kivukoni Kinondoni kutolewa kukamtwa kwa mabari mawili likiwemo moja kubwa lililotolewa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro. Awali deni hilo lilikuwa ni shilingi milioni 21 lakini kuchelewa kulipwa kwa deni hilo kumepelekea deni hilo kufikia shilingi milioni 51. Hata hivyo baada ya mazungumzo marefu baina ya katibu wa TFF Angetile Oseah na maafisa wa kampuni ya Flamingo hatimaye basi hilo lilinusurika kuondolewa kwa kile kilichoelezwa kuwa TFF ilipunguza deni hilo kwa pesa taslimu. |
|
Basi la TFF aina ya Coaster kama lilivyokuwa likipigwa picha na waandishi wa habari. |
No comments:
Post a Comment