KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 10, 2014

Serikali yawataka wasimamizi wa ligi nchini Ufaransa kuchukua hatua dhidi ya mashabiki

SERIKALI ya Ufaransa imewataka wasimamizi wa ligi nchini Ufaransa (LFP) kuchukua hatua kufuatia vurugu zilizojitokeza hapo jana katika mchezo baina ya Bastia na Marseille.

Polisi walipambana na mashabiki nje ya uwanja kabla na baada ya mchezo huo wa ligi kuu nchini humo maarufu kama League 1 uliofanyika Corsica, ambapo mashabiki walikuwa wakitupa mawe na miripuko.

Taarifa ya serikali imesema vurugu hizo zimesababisha jumla ya maafisa 44 wa polisi kujeruhiwa.

Katika mchezo huo nyota wa Marseille Andre-Pierre Gignac alifunga mara mbili na matokeo ya mwisho ya mchezo yakisomeka sare ya 3-3
Bastia aliamuriwa kucheza michezo miwili dhidi ya Marseille na Ajaccio bila ya watazamaji msimu uliopita kufuatia vurugu za mashabiki wake wakati na baada ya mchezo huko Corsican na hiyo ilikuwa ni mwezi March 2013.

Klabu hiyo huko nyuma iliwahi kuingia matatizoni na mamlaka ya ligi hiyo (LFP) kufuatia mashabiki wake kuonyesha mabango yenye dhihaka ya kibaguzi katika uwanja wake wa nyumbani.