KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 10, 2014

Mashabiki wa Liverpool wanakerekwa na kuendelea kumuona Luis Suarez Anfield kuelekea kuanza kwa msimu kisa anauza jezi za msimu mpya


Inavyoonekana ni kwamba Liverpool inashindwa kupambanua mambo ya kimsingi ya kimakubaliano tangu kuondoka kwa Luis Suarez kwani mpaka hivi sasa ni kwamba uwanja wa Anfield bado unaendelea kumuonyesha mshambuliaji huyo raia wa Uruguay katika bango kubwa lililoko lango kuu la kuingilia uwanjani hapo(Kop stand.

Ingawaje ni mwezi sasa umepita tangu taarifa za kuondoka kwake na hata baada ya kuondoka na kujiunga na Barcelona, bado mshambuliaji huyo ameendelea kutangaza vifaa vipya vya klabu hiyo langoni hapo akiwa katika jezi mpya ya msimu huu mpaka kufikia katika mchezo wa leo wa kikosi cha Brendan Rodgers kikishuka uwanjani dhidi ya Borussia Dortmund.

Mshabiki wanasema Suarez ataendelea kuonekana Anfield kama vile ishara ya kuendeleza uwepo wake akiitangaza jezi mpya kupitia bango hilo.
Jumapili ijao Liverpool itakuwa ikifungua msimu dhidi ya Southampton, sasa mashabiki wanasema ifanyike haraka kuondoa tangazo hilo kabla ya mchezo wa Jumapili.