KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 10, 2014

Eliaquim Mangala atajwa na Pellegrini kuwa kikosini Manchester City msimu huu

Eliaquim Mangala atajwa na Pellegrini kuwa kikosini Manchester City msimu huu
Manuel Pellegrini amedai kuwa Eliaquim Mangala tayari nim mchezaji wa Manchester City.
Mlinzi huyo wa Porto alikuwa katika tetesi za kuelekea Etihad Stadium kwa uhamisho wa pauni milioni 32 huku taarifa zikisema kuwa mpango huo ulikuwa ukikwamishwa na upande wa tatu wa mmiliki wa mchezaji huyo.
Duru zainaarifu kuwa mlinzi huyo mwenye uwezo wa kucheza sehemu mbalimbali za ulinzi uwanjani alikubali mpango wa kujiunga na City mara tu aliporejea akitokea katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil lakini mambo ya fedha yakawa ni kikwazo.
Katika mahojiano kabla ya kuelekea katika mchezo wa ngao ya jamii hii leo Pellegrini alimtaja Mangala kuwa ni miongoni mwa wachezaji wake watakao kuwemo kikosini msimu huu sambamba na Bacary Sagna, Willy Caballero na nyota wa zamani wa Porto mwenye umri wa miaka 23 Fernando.