Ilikuwa ni siku ya kwanza akiingia kazini kama meneja wa United ndani ya viunga vya uwanja wa mazoezi vya Carrington |
Wamiliki wa klabu hiyo kundi maarufu la 'Glazer family' hatimaye limepoteza uvumilivu kwa Moyes baada ya mabingwa hao watetezi wa taji la ligi ya Barclays Premier kuendelea kushikilia nafasi ya saba katika msimamo wa ligi.
Maumivu ya mwisho yalikuja jumapili iliyopita ambapo walichapwa mabao 2-0 matokeo ambayo yamewaweka nyuma kwa alama 13 kuifikia nafasi ya ligi ya mabingwa Ulaya.
The Glazers na mtendaji mkuu Ed Woodward walitarajiwa kuonyesha uvumilivu kwa Moyes lakini imeonekana wazi kuwa kuna kila dalili kuwa kiwango cha timu kimezidi kuwa kibaya na kwamba wachezaji wameacha kumpigania meneja wao.
Imefahamika kuwa mpango uliopo ni kumfukuza kazi Moyes mwishoni mwa msimu lakini hali ilivyo inaonekana ni jambo ambalo linaweza kutoka hata leo au siku chache zijazo.
Endapo bosi huyo wa zamani wa Everton atafukuzwa kabla ya kumalizika msimu mchezaji mkongwe wa klabu hiyo Ryan Giggs huenda akakabidhiwa jukumu la mambo ya timu.
Kuhusu ni nani wa kuchukua nafasi yake kwa kipindi kirefu kijacho, ni kwamba meneja wa sasa wa Dortmund Jurgen Klopp,
mkocha wa Uholanzi Louis van Gaal na kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti wako katika mpango huo.
Licha ya usajili wa gharama aliofanya kwa wachezaji Marouane Fellaini majira ya kiangazi iliyopita,lakini pia mwezi mwezi Januari kumchukua Juan Mata, United imeshindwa kuendeleza moto wake ikiwa ni pamoja na kukabiliana na wapinzani wake kiasi kupambana katika changamoto ya kutetea taji.
Moyes, ambaye alijiunga na United akitokea Everton majira ya kiangazi akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, ameshuhudia mwenyewe kushindwa katika mashindano mbalimbali.
United
ilitolewa na Swansea City katika roundi ya tatu ya michuano ya FA, ikatolewa tena na Sunderland katika nusu fainali ya Capital One,kabla ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na Bayern
Munich.
Ukichukuliwa katika michuano yote United imeshinda michezo 27 kati ya michezo 51 katika kipindi cha uongozi wa Moyes, ikienda sare mara tisa na kufungwa michezo 15.
No comments:
Post a Comment