KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 19, 2014

Yanga na Simba hakuna mbabe, mchezo ulikuwa na mvuto zaidi ya michezo yao miwili iliyopita

Mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya waliokuwa mabingwa wa soka msimu uliopita Yanga dhidi ya Simba umemalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1.

Sare hiyo imemaliza tambo miongoni mwao za kabla ya ya mchezo na sasa hakuna wa kumtambia mwenzake tena baada ya sare hiyo ya kufunga Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, leo.

Mabao yote yamepatikana katika kipindi cha pili tena dakika 10 za mwisho baada ya Simba kufunga lao katika dakika ya 82 kupitia Haruna Chanongo.
 
Lakini Yanga, wakasawazisha dakika ya 85 kupitia kwa Simon Msuva aliyepokea pasi ya Didier Kavumbagu.


Mechi hiyo ilikuwa na vivutio vingi na Simba walionekana kuutawala mpira katika kipindi cha kwanza.
 
Huo ulikuwa ni mchezo ambao umehitimisha ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu ambapo Yanga wamemaliza katika nafasi ya pili wakiwa na alama 56. 

No comments:

Post a Comment