KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 19, 2014

Azam fc watakata Chamazi, Jamali Malinzi awakabidhi Kombe na cheti kutoka FIFA kwa Blatter, wamaliza ligi bila kufungwa

Wachezaji wa Azam wakisherehekea na taji lao baada ya kukabidhiwa

AZAM FC imetimiza ndoto za kumaliza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bila kupoteza mechi baada ya ushindi wa 1-0 jioni hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Shukrani kwake Mganda, Brian Umony aliyefunga bao hilo dakika ya 70 na kwa matokeo hayo, Azam FC inamaliza na pointi 62 na wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Bara, wakiipokonya taji Yanga SC iliyomaliza katika nafasi ya pili na pointi 56 baada ya sare ya 1-1 jioni hii na watani wao, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam ilijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Jumapili iliyopita, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kufikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi ambazo zisingeweza kufikiwa na t

Licha ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Aprili 13, mwaka huu, Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo
Azam inakuwa timu ya saba nje ya Simba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Pan Africans mwaka 1982, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.

Mechi ya leo ilihudhuria na Wakurugenzi wake, Abubakar, Omar na Yussuf Bakhresa ambao waliketi jukwaa kuu pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Malinzi alimkabidhi Kombe la ubingwa Nahodha wa Azam, John Bocco baada ya mechi hiyo pamoja na cheti maalum kutoka FIFA, ambacho kinatolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu na Azam inakuwa timu ya kwanza kupata.

Wachezaji wote walivalishwa Medali baada ya mechi na baada ya hapo sherehe za ubingwa zilichukua nafasi yake Uwanja wa Azam Complex.

No comments:

Post a Comment