Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema mabingwa
hao wa Ulaya sharti waonyeshe sifa za klabu yao “Wanyama weusi”
watakapokutana na Real Madrid Jumatano kwenye mechi ya kwanza ya
nusu fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mashabiki wa Real wamewapa Bayern jina la utani la "la bestia negra"
(Wanyama weusi) au "Bete Noire" kufuatia msururu wa vichapo kutoka kwa
miamba hao wa Ujerumani, huku juzi zaidi kikiwa nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa 2012, ambayo iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti Madrid.
Bayern wameshuka kiwango chao cha uchezaji, wameshinda mechi tatu kati ya saba
walizocheza majuzi tangu washinde taji la Bundesliga mwezi jana wakiwa
wamesalia na mechi saba za kucheza, ambayo ni rekodi.
Rummenigge anataka
kuonya timu hiyo ikionyesha ukali wake zaidi Madrid.
"Tunajulikana kama 'la bestia negra' huko na tunahitaji kuwaonyesha
kwamba 'la bestia negra' wamerudi," akasema Rummenigge baada ya ushindi
wa Bayern usio wa kuridhisha wa 2-0 katika Bundesliga dhidi ya timu
inayoshika mkia ya Eintracht Braunschweig Jumamosi.
Rummenigge amewataka wachezaji hao wawe na ujasiri – na wapate angalau bao moja la ugenini mechi hiyo ya kwanza Madrid.
“Tunahitaji kufunga angalao goli moja. Hayo ndiyo tulijifunza kutoka
kwa mechi za Dortmund na Real Madrid,” akaongeza baada ya Borussia
Dortmund kubanduliwa kutoka Ligi ya Mabingwa, licha ya ushindi wa 2-0
robofainali nyumbani, baada yao kushindwa 3-0 wakiwa Madrid.
Bayern waliimarishwa Jumapili baada ya kipa wa Ujerumani Manuel Neuer
kurudi mazoezini baada ya kukosa mechi mbili zilizotangulia kutokana na
jeraha la misuli ya chini ya mguu na pia beki wa kushoto David Alaba
aliyerudi baada ya kukosa mechi ya Braunschweig kutokana na mafua.
Bado haijabainika kama nyota wa Real Cristiano Ronaldo atakuwa sawa
kucheza mechi hiyo ya Bernabeu, lakini Rummenigge amesema anapenda sana
nyota huyo wa Ureno aongoze mashambulizi ya Real wakiwa Madrid.
"Mechi hiyo ya nusufainali ni kubwa na itatazamwa na watu kila pembe
ya dunia. Kwa hivyo tunataka kuona wachezaji wote wazuri,” akaongeza
Rummenigge.
No comments:
Post a Comment