KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 5, 2014

Ligi kuu Tanzania Bara: Simba na Mtibwa waenda sare Jamhuri Morogoro

Mtibwa Sugar imeipunguza kasi Simba baada ya kutoka nayo sare ya bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja Jamhuri mjini Morogoro.

Mechi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ilikuwa ni ya Mtibwa Sugar katika kipindi cha kwanza ambayo ilianza kupata bao kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi.
Mgosi, mshambuliaji wa zamani wa Simba alifunga bao hilo baada ya kuiwahi krosi iliyochongwa safi na kupiga kichwa kilichomzidi Ivo Mapunda.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili, Simba iliposawasiaha kupitia Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga bao lake la 14 katika ligi hiyo.
Baadaye kiungo mkongwe wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi alilambwa kadi nyekundu kwa madai alimtolea lugha chafu mwamuzi Donisya Nkurya wa Arusha.
Kabla ya mechi hiyo, Simba iliiadhibu JKT Oljoro kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kabla ilikuwa imeichapa Rhino ya Tabora, bao -10 kwenye uwanja huo.

No comments:

Post a Comment