KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 21, 2012

DIONIZ MALINZI: ANNA KIBIRA HANA MATATIZO ANAWEZA KUGOMBEA UONGOZI CHANNETA.

Dioniz Malinzi mwenyekiti wa BMT.
  Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemuondolea adhabu ya kifungo cha muda usiojulikana katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira kufuatia baraza hilo kubaini kuwa hana hatia yoyote.

Taarifa kutoka ndani ya BMT zimeeleza kuwa sasa, Kibira yuko huru na kwamba, akitaka anaweza kujitosa katika kuwania uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa Chaneta utakaofanyika hivi karibuni.

  Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi, amesema Kibira yuko huru na kwamba kuanzia sasa anaweza kugombea nafasi yoyote anayoitaka kutokana na ukweli kwamba hana hatia inayomzuia kugombea katika uchaguzi mkuu wa chama hicho.

 Amesema kuanzia sasa, Kibira na wanamichezo wengine wenye nia ya kugombea wanapaswa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho.

 Aliongeza kuwa Kibira anatarajiwa kufika kwenye ofisi za BMT kuanzia leo kupata maelekezo kutokana na adhabu aliyokuwa amepewa awali na kamati ya utendaji ya CHANETA, ambayo iliashiria kufungiwa kwake kwa muda usiojulikana.

 Aidha, Kibira amesema kuwa bado hajapata taarifa yoyote kuhusiana na kufungiwa kwake Chaneta, lakini amefurahishwa na uamuzi wa kuondolewa adhabu na kwamba atakuwa tayari kutangaza nia yake pale atakapopata uthibitisho rasmi kuwa yuko huru kugombea katika uchaguzi huo.
Anna Kibira katibu wa zamani wa CHANETA.
  "Nimefurahi kusikia hivyo. Lakini nasubiri taarifa rasmi kutoka kwa BMT ili nijihakikishie kama kweli ninaruhusiwa kugombea," amesema Kibira.

 Aliongeza kuwa, katika muda wote wa kusimamishwa kwake CHANETA, amekuwa akijishughulisha na michezo mingine kutokana na ukweli kuwa michezo iko damuni.

Licha ya kufungiwa kwa muda usiojulikana, Kibira alikuwa hajawahi kupewa barua yoyote hadi BMT ilipoeleza jana kuwa yuko huru na kwamba sasa anaweza kujishughulisha na CHANETA

No comments:

Post a Comment