Hivi shirikisho la soka Afrika
mashariki na kati CECAFA ni mna maslahi na Issa Hayatou ambaye ijumaa
mlikubaliana kumuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwezi machi nchini Morocco.
Hayatou ameingia
madarakani tangu mwaka 1986 vijana wengi wanaocheza mpira hii leo walikuwa bado
hawajazaliwa hii leo ni miaka 25 imepita
anawaomba kura zenu na ninyi mna muunga mkono kwa kauli moja bila kujiuliza
mzee huyu kawaletea nini cha kimaendeleo katika ukanda wenu ambao umezidi
kudumaa kisoka.
Safari yake ya
kuongoza soka Afrika kwa muda wote huo haina la kujivunia kwetu maana hakuna
taji hata moja kubwa katika ukanda wenu si taji la mataifa ya Afrika CAN wa
vilabu wala mataji ya vilabu tangu kufanywa hivyo kwa mara ya mwisho na Gor Mahia ya Kenya mwaka
1987.
Mnajivunia maendeleo,
hayo maendeleo ni yapi wakuu wangu wa soka mbona kichekesho kama miradi ya
ujenzi wa viwanja vingi hufanywa na serikali zetu moja kwa moja kwa
kushirikiana na mataifa marafiki na si mkono wa CAF, sasa kama hiyo ni hoja yake mbona haina
mashiko.
Kama ni
miradi ya elimu kwa makocha na waamuzi
kujenga uwezo wa wakufunzi wetu hilo limo ndani ya sera za CAF na katiba yake sambamba na mipango
ya maendeleo ya shirikisho lakini pia ni kwa bara zima la Afrika na si jambo la
Hayatou pekee yake.
Kinachonishangaza
ni kwamba ujio wake Afrika mashariki umefanyika katika kipindi ambacho kuna
michuano ya mataifa yetu ya Afrika mashariki na kati halafu amechungulia uchaguzi mwezi machi mwakani.
Hivi hawezi kuwatembelea
wapiga kura wake mpaka kipindi kama hiki cha mashindano na uchaguzi kesho?
Wenzetu wa Afrika magharibi kinachowasumbua hawapendi utawala wa kupokezana vijiti jambo ambalo wanalifanya liwe kawaida na ndio maana kila kukicha wanabadilisha sheria na kanuni ili kuziba mianya ya wadau wengine kuongoza.
Nasema hivi kwasababu hivi karibuni CAF wamebadilisha sheria moja muhimu sana hasa baada ya michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Wapo watu waliochomoza na kuongoza vizuri sana maandalizi na uendeshaji wa fainali zile na hivyo kuonekana kama tishio kwa Hayatou akiwemo aliyekuwa mtendaji mkuu wa kombe la dunia Danny Jordaan pamoja na Jacques Anouma ambaye ni mjumbe katika kamati ya bodi ya utawala ya shirikisho la soka duniani FIFA.
Wamefanya siasa na fitna kubwa kufanyia mabadiliko sheria za CAF ili zibadilishwe kwa lengo la kuwaweka hawa jamaa nje ya harakati za kugombea Urais wa CAF na kwa ujinga wa wanachama wa CAF ambao walitekwa akili kwenye mkutano wa Seychelles mapema mwezi june mwaka huu, hilo likakubalika lakini ukilitazama kwa umakini ni fitna tu kutaka watu waendelee kutawala.
Leo hii Hayatou anakuja Afrika Mashariki na kati na kuingia kwenye kikao cha Cogress na kutumia fursa hiyo kuomba kura za kuungwa mkono katika uchaguzi wa mwezi machi nchini Morocco na viongozi wetu wa soka wanakubali kumuunga mkono bila hoja bila maswali, mmeonyesha udhaifu mkubwa sana.
Wenzetu wa kanda nyingine wana hoja na wana mashinikizo wanapo taka mambo yao ya msingi yafanyiwe kazi na si kupewa kupewa pipi na peremende.
Miradi mingi ya maendeleo barani Afrika inatoka FIFA na si CAF ambao wamezidi blah blah nyingi na posho wanachama wao na wakurugenzi wa ufundi wa vyama wanachama wao.
Binafsi siungi mkono kura zenu kwa Hayatou kwasababu kubwa mbili kwanza Hayatou anaunga mkono sana maendeleo ya soka ukanda wa magharibi na ndio maana sehemu kubwa ya utawala wake katika soka Afrika imetawaliwa na nchi za Afrika Magharibi.
Nchi hizo ni Nigeria, Misri , Cameroon, Algeria, Morroco, Tunisia na Ivory Coast ukiacha Afrika Kusini ambao uchumi wa nchi yao ni imara.
Issa Hayatou hafanyi ziara kwa nchi wanachama wake kujua mipango yao ya maendeleo zaidi ya kutuma ujumbe wake, ambao nao unachukua muda mrefu kutembelea wanachama tofauti na Ulaya ambako kila siku utasikia Michel Platin anatembelea wanachama wa EUFA akikagua miradi ya maendeleo ya soka barani humo licha ya utajiri wa mataifa hayo.
Imenisikitisha sana Ijumaa kusikia kuwa baraza
la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (Cecafa) limeamua kumuunga mkono
Rais wa sasa wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou katika
kampeni yake ya kutaka kuongoza tena shirikisho hilo.
Kumbuka uchaguzi
wa CAF utafanyika mwezi Machi nchini Morocco.
Maamuzi ya Cecafa
yamekuja katika kikao cha congress kilicho fanyika ijumaa ambapo bodi iliamua
kwa kauli moja kumuunga mkono Hayatou kwasababu ya rekodi yake mpaka alipofikia
hususani katika maendeleo ya mpira wa miguu.
Rais wa
shirikisho la soka la Kenya Sam Nyamweya alinukuliwa akisema
"tumeamua
kumuuunga mkono Hayatou kwa mara nyingine tena ili amalizie yale aliyo
yaanzisha na kumshukuru kwa yale aliyoyafanya,"
Akaendelea kwa
kusema Hayatou amesaidia kuleta kombe la dunia Afrika kwa mara ya kwanza
tumepata wadhamini wengi katika soka lakini pia ameanzisha michuano ya fainali
za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika CHAN leza wachezaji wa
ndani.
Kwa maneno
hayo ni kwamba kura za nchi wanachama wa CECAFA zote 12 zinakwenda kwa Hayatou
ambazo ni Uganda,Kenya,Tanzania,Rwanda,Burundi,Djibouti,
Sudan, South Sudan,Ethiopia,Somalia na Eritrea.
Hayatou
alikuwa na baadhi ya wajumbe wa Caf ambao walimpa kampani kwenye kikao cha kongresi cha cecafa.
Mwingine ni
katibu mkuu wa shirikisho la soka la Somalia (SFF), Abdi Qani Said Arab, amenukuliwa
na BBC akisema itakuwa vizuri kwa Cecafa kumuunga mkono Hayatou kwasababu
ameleta mafanikio mengi katika bara hili na ndio mgombea pekee.
Hivi karibuni
shirikisho la soka barani Afrika Caf lilipitisha sheria mpya ambayo kimsingi
inawakataza watu wan je ya kamati ya utendaji kugombea Urais wa shirikisho hilo.
Hiyo maana
yake ni kwamba Jacques Anouma, mmoja wa wawakilishi wa kamati ya utendaji ya
bodi ya utawala ya Fifa, na mtendaji mkuu wa maandalizi ya kombe la dunia mwaka
2010 nchini Afrika Kusini Danny Jordaan kuwa hawana nafasi ya kugombea nafasi
hiyo.
Mabadiliko hayo
yanapelekea kwamba mtu yoyote anayetaka Urais lazima awe mwanachama mpiga kura
kutoka kamati ya utendaji. Hii maana yake ni kuwa awe na kura ambayo
inatambuliwa na CAF kwa maana nyingine awe kiongozi ndani ya chama mwanachama
wa CAF.
Huku ni kutokujiamini kwa watu wa mpira wa ukanda wa Afrika mashariki na si dhani kama Hayatou anamzidi saaana akili ya kuongoza mpira wa miguu Nyamwea na Tenga hapo ni suala la utashi tu na kuthubutu.
Tutabaki kuwa wasindikizaji miaka yote wenzetu wanatukandamiza na ukanda wetu unazidi kuonekana hamna kitu kila siku.
Hayatou amekuwa
Rais wa Caf tangu mwaka 1987. Mwaka 2002, aligombea urais wa Fifa lakini
alishindwa na rais wa sasa Sepp Blatter.
Ndiye Rais mkongwe kuliko marais wote wanaonongoza masharikisho ya soka duniani na sasa anataka tena kipindi kingine cha miaka minne.
Asante sana kwa kuwa unatuhabarisha katika masuala mbalimbali ya soka na michezo mingine na habari mbalimbali lakini katika sula la Issa Haytou hukuweza kujua jambo moja la muhimu sana , najua kabisa una midadi ya soka kwamba siku moja iwe kama ulaya inawezekana kabisa lakini siku zote maendeleo yanahitaji mipango na walichokifanya CECAFA ni muhimu mno kwa kumweka karibu. Unajua kabisa hata nchini Tanzania kuna watu wana uwezo zaidi yako lakini kwasababau hawako karibu hawaonekani kabisa hivyo kujitenga sio suluhu hata kidogo. TUSIWE WATU WA KULAUMU NA KUTAKA MAMBO FASTA FASTA. Thanks.
ReplyDelete