KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 25, 2012

NYIE CECAFA HUYU HAYATOU KAWASAIDI NINI AFRIKA MASHARIKI NA KATI? KWANINI MNA MFANYA MFALME WA SOKA LA AFRIKA.




Rais wa Cecafa Leodgar Tenga akizungumza na kiongozi wa FA ya Kenya Sam Nyamweya (kushoto) na Rais wa shirikisho la soka Uganda (FUFA) President Lawrence Mulindwa kwenye kikao cha Congress cha cecafa.
  Hivi shirikisho la soka Afrika mashariki na kati CECAFA ni mna maslahi na Issa Hayatou ambaye ijumaa mlikubaliana kumuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwezi machi nchini Morocco.
Hayatou ameingia madarakani tangu mwaka 1986 vijana wengi wanaocheza mpira hii leo walikuwa bado hawajazaliwa  hii leo ni miaka 25 imepita anawaomba kura zenu na ninyi mna muunga mkono kwa kauli moja bila kujiuliza mzee huyu kawaletea nini cha kimaendeleo katika ukanda wenu ambao umezidi kudumaa kisoka.

Safari yake ya kuongoza soka Afrika kwa muda wote huo haina la kujivunia kwetu maana hakuna taji hata moja kubwa katika ukanda wenu si taji la mataifa ya Afrika CAN wa vilabu wala mataji ya vilabu tangu kufanywa hivyo kwa mara ya mwisho na Gor Mahia ya Kenya mwaka 1987.

Mnajivunia maendeleo, hayo maendeleo ni yapi wakuu wangu wa soka mbona kichekesho kama miradi ya ujenzi wa viwanja vingi hufanywa na serikali zetu moja kwa moja kwa kushirikiana na mataifa marafiki na si mkono wa CAF,  sasa kama hiyo ni hoja yake mbona haina mashiko.

Kama ni miradi ya elimu kwa makocha na waamuzi  kujenga uwezo wa wakufunzi wetu hilo limo ndani ya sera za CAF na  katiba yake sambamba na mipango ya maendeleo ya shirikisho lakini pia ni kwa bara zima la Afrika na si jambo la Hayatou pekee yake.

Kinachonishangaza ni kwamba ujio wake Afrika mashariki umefanyika katika kipindi ambacho kuna michuano ya mataifa yetu ya Afrika mashariki na kati halafu amechungulia uchaguzi mwezi machi mwakani.

 Hivi hawezi kuwatembelea wapiga kura wake mpaka kipindi kama hiki cha mashindano na uchaguzi kesho?

Wenzetu wa Afrika magharibi kinachowasumbua hawapendi utawala wa kupokezana vijiti jambo ambalo wanalifanya liwe kawaida na ndio maana kila kukicha wanabadilisha sheria na kanuni ili kuziba mianya ya wadau wengine kuongoza.

Nasema hivi kwasababu hivi karibuni CAF wamebadilisha sheria moja muhimu sana hasa baada ya michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wapo watu waliochomoza na kuongoza vizuri sana maandalizi na uendeshaji wa fainali zile na hivyo kuonekana kama tishio kwa Hayatou akiwemo aliyekuwa mtendaji mkuu wa kombe la dunia Danny Jordaan pamoja na Jacques Anouma ambaye ni mjumbe katika kamati ya bodi ya utawala ya shirikisho la soka duniani FIFA.

Wamefanya siasa na fitna kubwa kufanyia mabadiliko sheria za CAF ili zibadilishwe kwa lengo la kuwaweka hawa jamaa nje ya harakati za kugombea Urais wa CAF na kwa ujinga wa wanachama wa CAF ambao walitekwa akili kwenye mkutano wa Seychelles mapema mwezi june mwaka huu,  hilo likakubalika lakini ukilitazama kwa umakini ni fitna tu kutaka watu waendelee kutawala.

Leo hii Hayatou anakuja Afrika Mashariki na kati na kuingia kwenye kikao cha Cogress na kutumia fursa hiyo kuomba kura za kuungwa mkono katika uchaguzi wa mwezi machi nchini Morocco na viongozi wetu wa soka wanakubali kumuunga mkono bila hoja bila maswali, mmeonyesha udhaifu mkubwa sana. 

Wenzetu wa kanda nyingine wana hoja na wana mashinikizo wanapo taka mambo yao ya msingi yafanyiwe kazi na si kupewa kupewa pipi na peremende.  

Miradi mingi ya maendeleo barani Afrika inatoka FIFA na si CAF ambao wamezidi blah blah nyingi na posho wanachama wao na wakurugenzi wa ufundi wa vyama wanachama wao.

Binafsi siungi mkono kura zenu kwa Hayatou kwasababu kubwa mbili kwanza Hayatou anaunga mkono sana maendeleo ya soka ukanda wa magharibi na ndio maana sehemu kubwa ya utawala wake katika soka Afrika imetawaliwa na nchi za Afrika Magharibi.

Nchi hizo ni Nigeria, Misri , Cameroon, Algeria, Morroco, Tunisia na Ivory Coast ukiacha Afrika Kusini ambao uchumi wa nchi yao ni imara.

Issa Hayatou hafanyi ziara kwa nchi wanachama wake kujua mipango yao ya maendeleo zaidi ya kutuma ujumbe wake, ambao nao unachukua muda mrefu kutembelea wanachama tofauti na Ulaya ambako kila siku utasikia Michel Platin anatembelea wanachama wa EUFA akikagua miradi ya maendeleo ya soka barani humo licha ya utajiri wa mataifa hayo. 
 

 Imenisikitisha sana Ijumaa kusikia kuwa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (Cecafa) limeamua kumuunga mkono Rais wa sasa wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou katika kampeni yake ya kutaka kuongoza tena shirikisho hilo.

Kumbuka uchaguzi wa CAF utafanyika mwezi Machi nchini Morocco.

Maamuzi ya Cecafa yamekuja katika kikao cha congress kilicho fanyika ijumaa ambapo bodi iliamua kwa kauli moja kumuunga mkono Hayatou kwasababu ya rekodi yake mpaka alipofikia hususani katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Rais wa shirikisho la soka la Kenya Sam Nyamweya alinukuliwa akisema 

"tumeamua kumuuunga mkono Hayatou kwa mara nyingine tena ili amalizie yale aliyo yaanzisha na kumshukuru kwa yale aliyoyafanya," 

Akaendelea kwa kusema Hayatou amesaidia kuleta kombe la dunia Afrika kwa mara ya kwanza tumepata wadhamini wengi katika soka lakini pia ameanzisha michuano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika CHAN leza wachezaji wa ndani.

Kwa maneno hayo ni kwamba kura za nchi wanachama wa CECAFA zote 12 zinakwenda kwa Hayatou ambazo ni  Uganda,Kenya,Tanzania,Rwanda,Burundi,Djibouti, Sudan, South Sudan,Ethiopia,Somalia na Eritrea.

Hayatou alikuwa na baadhi ya wajumbe wa Caf ambao walimpa kampani kwenye kikao cha kongresi cha cecafa.

Mwingine ni katibu mkuu wa shirikisho la soka la Somalia (SFF), Abdi Qani Said Arab, amenukuliwa na BBC akisema itakuwa vizuri kwa Cecafa kumuunga mkono Hayatou kwasababu ameleta mafanikio mengi katika bara hili na ndio mgombea pekee.

Hivi karibuni shirikisho la soka barani Afrika Caf lilipitisha sheria mpya ambayo kimsingi inawakataza watu wan je ya kamati ya utendaji kugombea Urais wa shirikisho hilo.

Hiyo maana yake ni kwamba Jacques Anouma, mmoja wa wawakilishi wa kamati ya utendaji ya bodi ya utawala ya Fifa, na mtendaji mkuu wa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini Danny Jordaan kuwa hawana nafasi ya kugombea nafasi hiyo.

Mabadiliko hayo yanapelekea kwamba mtu yoyote anayetaka Urais lazima awe mwanachama mpiga kura kutoka kamati ya utendaji. Hii maana yake ni kuwa awe na kura ambayo inatambuliwa na CAF kwa maana nyingine awe kiongozi ndani ya chama mwanachama wa CAF.

Huku ni kutokujiamini kwa watu wa mpira wa ukanda wa Afrika mashariki na si dhani kama Hayatou anamzidi saaana akili ya kuongoza mpira wa miguu Nyamwea na Tenga hapo ni suala la utashi tu na kuthubutu.

Tutabaki kuwa wasindikizaji miaka yote wenzetu wanatukandamiza na ukanda wetu unazidi kuonekana hamna kitu kila siku. 


Hayatou amekuwa Rais wa Caf tangu mwaka 1987. Mwaka 2002, aligombea urais wa Fifa lakini alishindwa na rais wa sasa Sepp Blatter.

Ndiye Rais mkongwe kuliko marais wote wanaonongoza masharikisho ya soka duniani na sasa anataka tena kipindi kingine cha miaka minne.

1 comment:

  1. Asante sana kwa kuwa unatuhabarisha katika masuala mbalimbali ya soka na michezo mingine na habari mbalimbali lakini katika sula la Issa Haytou hukuweza kujua jambo moja la muhimu sana , najua kabisa una midadi ya soka kwamba siku moja iwe kama ulaya inawezekana kabisa lakini siku zote maendeleo yanahitaji mipango na walichokifanya CECAFA ni muhimu mno kwa kumweka karibu. Unajua kabisa hata nchini Tanzania kuna watu wana uwezo zaidi yako lakini kwasababau hawako karibu hawaonekani kabisa hivyo kujitenga sio suluhu hata kidogo. TUSIWE WATU WA KULAUMU NA KUTAKA MAMBO FASTA FASTA. Thanks.

    ReplyDelete