KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, April 17, 2014

Kocha Gordon Igesund wa Afrika kusini avualiwa tuhuma licha ya mkataka wake kuelekea kumalizika mwezi Juni

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika kusini Gordon Igesund amesafishwa kutoka kwenye tyhuma zilizokuwa zinamkabili huko nyuma kuwa alichochea mgomo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo Bafana Bafana waliokuwa wakielekea kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN mwaka 2014.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Johannesburg hii leo chama cha soka nchini humo kimesema tuhuma dhidi ya kocha huyo zilikuwa hazina msingi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 ambaye amekuwa kibaruani tangu mwaka 2012, mara kadhaa amekuwa akikanusha madai hayo, na sasa yuko huru kuendelea na makataba ambayo unatarajiwa kumalizika Juni mwaka huu.

Hii ina maana kuwa atakuwa akiendelea na kikosi hicho ambacho kitakuwa na ziara ya michezo miwili mwezi ujao lakini inawezeakana kuwa atakuwa anamalizia kazi yake kama kocha wa Bafana Bafana  kufuatia kushindwa kufanya vizuri katika fainali za mapema mwaka huu CHAN.

Afrika Kusini inatarajjiwa kuajiri kocha mpya mwezi Juni ili kumpa muda zaidi wa kuandaa kikosi kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali zijazo za mataifa ya Afrika 2015 kuanzia September. 

No comments:

Post a Comment