Saidi Bahanuzi akiongea na Rockersports |
Bahanuzi akiwa na mwandishi wa habari wa Uhuru fm na Rockersports Fatma Likwata |
Bahanuzi akimsikiliza kwa makini Limonga Justine katika mahojiano. |
Hapa akiwa na kashushu |
Rockersports
imetembelewa na kupata nafasi ya kufanya mahojiano na mshambuliaji mabingwa wa
kombe la Kagame Yanga Said Bahanuzi aliyemaliza michuano hiyo akiwa na jumla ya mabao
sita.
Bahanuzi
ambaye ni mrefu kiasi mweusi na mwili wa kawaida kabisa tofauti na anavyoenekana
uwanjani ameelezea juu ya historia ya maisha yake katika soka lakini pia akitoa
siri ya nzito ya mafanikio yake katika michuano ya vilabu bingwa Afrika kashariki na kati
maarufu kama Kombe la Kagame.
Fuatilia
mahojiano hayo kuyajua mengi ya nyuma ya pazia kuhusu Saidi Bahanuzi
aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mtibwa ya Morogoro.
Rockersports:Assalam alaykum
Bahanuzi:Alekum msalaama warahmatul laah
wabarakatul.
Rockersports: Vipi imepanda lakini?
Bahanuzi:kama kawaida mi muislam lazima
ipande.
Rockersports: Haya bwana, kubwa tuambie nini
siri ya mafanikio yako ndani ya Yanga baada ya muda mfupi wa kujiunga na timu
hiyo
Bahanuzi:Siri kubwa ni maombi kwa mungu
lakini pia baraka ambazo zimetokana na mke
wangu kujifungua mototo wa kiume kabla ya michuano ya Kagame hususani siku
mbayo nikiwa uwanjani dhidi nya Express ya Uganda mchezo wa kirafiki ambaye nimempa
jina la Samir
Rockersports :Alaah hongera sana bwana, umempa
zawadi gani Samir baada ya michuano hiyo kuwa imemalizika ?
Bahanuzi:Nilitegemea kumpa zawadi ya kiatu
ambacho kingetokana na tuzo ya ufungaji bora lakini mwenyezi mungu hakupenda
lakini kwasasa nimempa tuzo yangu ya medali ya ufungaji bora na lile goli la
mwisho dhidi ya Azam ni zawadi yake pia
Rockersports :Kuna tofauti gani kati ya mtibwa timu
yako ya zamani na Yanga ambayo unaichezea kwasasa?
Bahanuzi:Mtibwa ni timu ndogo lakini Yanga ni
timu kubwa kama ilivyo Simba.
Rockersports:Jina lako limekuwa sasa hasa baada
ya Kombe la kagame kumalizika nini malengo yako?
Bahanuzi:Malengo namshukuru mungu malengo
yangu ilikuwa ni kucheza yanga au Simba ambazo ni timu kubwa hapa nchini lakini
kucheza timu ya taifa na vilevile kwenda kucheza soka nje ya nchi.
Rockeesports:Wengi wamekuwa wakichanganya juu ya wapi uliko zaliwa ukweli uko wapi maana kuna wengine wanasema wewe ni mzanzibar na
wengine hata wakikuhusisha na kuzaliwa Congo ukweli uko wapi?
Bahanuzi: Hahahahahaaaa mimi ni mtu wa Mwanza lakini nimetokea Kigoma,
baba ni mtu wa Kigoma na mama mtu wa Mwanza.
Rockersports:Historia yako ikoje katika kandanda
Bahanuzi:Nimeanzia Mwanza ambako ndiko niliko
zaliwa na kukulia nilikuwa nacheza mpira mtaani baada ya kumaliza shule.Baadaye
nikaja Kibaha kumfuata mama baada ya mama na baba kuachana kufuatia mama yangu kuhamia
Kibaha na baadaye nikaja Dar maeneo ya Ilala lakini muda mwingi nilikuwa Kibaha
kwa mama ambako nilikuwa naendelea kucheza timu za mtaani.
Nikiwa
kibaha alikuja mtu kutoka Zanzibar alikuwa anatafuta wachezaji kwenda kucheza
ligi daraja la pili kule Zanzibar akanichukua nikaenda Zanzibar ligi dara la
pili halafu ndipo Mtibwa waliponiona wakanifuata nikachezea msimu uliopita
kabla ya kuja kucheza Yanga.
Rockersports: Kwa maana hiyo wewe ni mtanzania
bara?
Bahanuzi: Ya mimi baba yangu ni mtu wa Kasulu
Kigoma na mama mtu wa Mwanza.
Rockersports:Kumekuwepo na tetesi kuwa wewe ni
Mzanzibar huko sasa ikatokezea timu za taifa zinachaguliwa na wewe ukapata
bahati ya kuchaguliwa utachezea timu ya upande gani Bara au Zanzibar?
Bahanuzi:Mimi ni mtanzania bara nitachezea timu
ya bara
Rockersports:Vipi ushindani katika kikosi cha Yanga
ambacho kinawachezaji wengi wazuri lakini wewe umeaminiwa sana na kocha Thom Saintfiet katika michauno
ya Kagame
Rockersports:Bado zijajua kwa kweli licha ya
kuaminiwa na kocha lakini ukweli ushindani ni mkubwa kuna wachezaji wengi
wazuri na wengine nimewakuta na ninawaheshimu, naomba mungu ili nipate namba ya
kucheza na sina imani sasa ila naomba mungu inshaalah anisaidie kwa kuwa nina
miezi miwili tu katika timu sijui kwa kweli kama nitapata namba .
Rockersports:Unawaeleza nini wana-Yanga na kwa
kuwa hivi sasa ni timu yenye malengo makubwa zaidi ukilanganisha na Mtibwa
Bahanuzi: Kwa Wana-yanga cha msingi
naomba uzima kwasababu ukiwa mzima unaweza kufanya kitu chochote na lakini pia kwa
watanzania kama nitaitwa katika timu ya taifa baada ya kuonekana naweza kutoa
mchango wangu basi nitafanya kwa kadri mungu anavyotaka kukakamilisha malengo.
Rockersports:Vipi kuhusu Samiri mototo wako wa
kiume ambaye umeamua kumpa tuzo ya Kagame unataka afuate nyayo zako kucheza
soka?
Bahanuzi:Kwanza apate elimu na baadaye achezea
mpira ndio ndoto yangu lakini kwanza elimu
Rockersports:Sasa umekuwa na jina kubwa kila sehemu kila mahala ni Bahanuzi
redioni, magazetini na kwenye mitandao ya kijamimi ni wewe tu unajisikiaje sasa
juu ya hilo?
Bahanuzi : Najisikia vizuri kwa kuwa nafanya
kitu kizuri na ni watu ndivo walivyo nipokea kwa hiyo namshukuru mungu na
waendelee kunisupport
Rockersports: Tukirudi uwanjani umekuwa ukilalamikiwa juu ya kuwa off-side mara kwa mara kiasi kuonekana
ndio kasoro kubwa kwako hujui kujipanga kwenye mstari wa off-side hiyo ndio kasoro yako kubwa ukiachana na mambo mengine ya
kiufundi unapigiwa filimbi ya off-side unalizungumziaje
hilo?
Bahanuzi:Sawa lakini mshambuliaji mzuri lazima
apigiwe filimbi ya off-side kwa kuwa
unakuwa na uchu wa kufunga magoli.
Rockersports:vipi maisha
yako mapya ndani ya Yanga unayaonaje?
Bahanuzi: Nashukuru mungu Yanga ni timu nzuri
na ninashukuru nina ishi vizuri na wenzangu tunapendana na tunashirikiana
lakini vile vile tunasaidiana sana namshukuru mungu sana.
rockersports:Vipi kuhusu michuano ya kagame
umeionaje?
Bahanuzi:Kagame ilikuwa ni michuano mikubwa
kwangu na ilikuwa migumu kwa hiyo kwangu ni historia na kwa kweli imenibadilisha
katika misha ya soka na nimejifunza kitu kipya kabisa katika mpira wa miguu.
Rockersports:Tunashukuru sana baba Samir kwa
kututembelea na kupata nafasi ya kuongea na wewe karibu tena endapo tukiwa na
lolote tunaomba ushirikiano wako bwana.
Bahanuzi: hahahahahahahaaaaa asante hakuna shaka nakushukuru pia na
wewe kwa mahojiano yako.
Rockersports: Msalimie mama Samir
Bahanuzi: zimefika
No comments:
Post a Comment