Nyota wa Manchester United Adnan Januzaj amepiga chini wito wa shirikisho la soka la Kosovo kwa ajili ya kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyi dhidi ya Haiti mchezo uliopangwa kuchezwa mwezi Marchi na hivyo kufungua mlango kwa England.
Mzaliwa huyo wa Brussels mwenye umri wa miaka 19, ambaye pia ana nafasi ya kuchaguliwa na mataifa ya Belgium na Albania, alialikwa na KFF kujiunga katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo mwezi ujao dhidi ya Haiti ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Pia vyanzo vya habari vilivyo karibu na mchezaji huyo kijana kabisa vimeliarifu gazeti la Telegraph kuwa mchezaji huyo hataweza kujiunga na kikosi cha Kosovo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kimataifa kwa taifa hilo tangu kujitangaza kuwa taifa huru mwaka 2008.
Januzaj ambaye amezaliwa na baba mwenye uraia wa nchi mbili yaani 'Kosovar-Albanian father' anayetambuliaka kwa jina la Abedin, anaonekana kama ndiye mwenye nafasi kubwa ya ushawishi kwa mwanae kuichezea Kosovo taifa ambalo halina uanachama wa Fifa ana ambalo halina nafasi ya kushiriki michezo ya kiushandani kokote zaidi ya michezo ya kirafiki.
Kwa upande wa familia imekuwa na joto kubwa juu ya wazo la Kosovo huku wakionekana dhahiri kupigia upatu wazo la Adan kuvalia jezi ya Simba Watatu yaani England.
No comments:
Post a Comment