![]() |
Rivaldo kushoto na Rivaldinho wakiichezea timu moja ya Mogi Mirim |
Rivaldo ameweka historia ya aina yake kwa kucheza kiwanja kimoja na mwanae wa kiume Rivaldinho.
Mwasisi huyo wa soka wa Brazil Rivaldo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 41, aliingia akitokea benchi akichukua nafasi katika timu yake ya Mogi Mirim katika mchezo wa ligi daraja la tatu mjini Sao
Paulo (Sao Paulo State league) ikiwa ni kwa mara ya kwanza anaungana na mwanae uwanjani mwenye umri wa miaka 18.
Huo ulikuwa ni mchezo dhidi ya XV
de Piracicaba uliopigwa Estadio Romildo Ferreira.
Rivaldo alishinda taji la kombe la dunia mwaka 2002 kikosi kikiwa chini ya Luiz Felipe Scolari na akiitumikia Brazil kwa michezo 74 akifunga mabao 34 kwa timu ya taifa.
Amewahi kuvichezea vilabu vya Barcelona, AC Milan, Deportivo La Coruna na
Olympiakos.
Nchini Brazil amewahi kuvichezea vilabu kama Corinthians na Palmeiras
kabla ya kujiunga na Mogi Mirim mwezi Disemba ambako sasa ameungana na mwanae Rivaldinho katika ligi ya daraja la tatu.
![]() |
Rivaldo mwaka 2002 |
No comments:
Post a Comment