KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, January 13, 2014

Breaking news Ballon d'Or: Cristiano Ronaldo awashinda Lionel Messi na Ribery

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuwashinda mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na Franck Ribery wa Bayern Munich katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo wa Fifa ya Ballon d'Or kwa mwaka 2013.
Nahodha huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 28, ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2008, alipigiwa kuara na makocha, manahodha na waandishi wa habari wa mchezo huo hii leo.
Mlinda mlango wa Ujerumani Nadine Angerer ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa tuzo za wanawake.
Kocha wa zamani wa Bayern Munich Jupp Heynckes amechukua nafasi ya kocha bora wa mwaka.
Messi mwenye umri wa miaka 26 alishinda tuzo hiyo mara nne mfululizo miaka minne iliyopita.

No comments:

Post a Comment