KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 26, 2012

BERNITEZ KAZI ANAYO



Benitez alijikuta katika wakati mgumu kwani alijikuta akikutana na upingwaji mkubwa kutoka kwa mashambiki wa timu hiyo ambao walionyesha wazi hasira zao dhidi ya meneja huyo wa zamani wa Liverpool ambaye amerithi nafasi ya Roberto Di Matteo.


Mchezo wa kwanza wa meneja Rafael Benitez akiwa kama meneja mpya wa klabu hiyo umemalizika kwa sare ya bila mabao dhidi ya Manchester City.

Mbaya zaidi meneja huyo mhispania alijikuta akishuhudia mchezo mbovu wa timu yake ambayo ilimudu kupiga shuti moja golini mchezo ambao uliwanyima raha mashabiki wengi.

Huku akishuhudiwa na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich,pengine kitu ambacho kimainusuru timu hiyo ni ulinzi mzuri wa sehemu ya ulinzi wa kati ambapo  David Luiz na Branislav Ivanovic walidhibiti vizuri mashambulizi na kupelekea kupunguza kelele za mashambiki wenye hasira.

No comments:

Post a Comment