Naibu waziri wa habari, Vijana, utamaduni na Michezo Juma
Nkamia hii leo amehudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha 'HISTORIA YA SIMBA' kilichotungwa na kuandiskwa na mwandishi mkongwe wa habari hapa nchini ambaye pia ni katibu wa zamani wa klabu ya Simba Mwina Mohamed Kaduguda uzinduzi uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi.
Akitoa hotuba ya iliyo kuwa na historia ndefu ya klabu ya Simba, waziri Nkamia alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa kitu kimoja katika kipindi hiki kwa lengo la
kuendeleza mambo mazuri na yenye mafanikio.
Nkamia amesema endapo wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo watashindwa kutimiza wajibu wao wa kuipenda klabu yao na kuithamini, kuna
hatari kubwa ya kukosekana kwa historia nzuri kwa miaka ijayo.
Hata hivyo Nkamia amempongeza muandishi wa kitabu hicho Mwina Seif Mohamed Kaduguda kwa kutumia ujasiri wake kwa kuweka kumbukumbu mbayo
katu haiwezi kufutika.
Kwa upande mtunzi wa kitabu hicho Kaduguda ambaye aliwahi kuwa katibu wa klabu ya Simba amesema ameamua kufanya
hivyo kutokana na wanachama na mashabiki wengi kutokuijua vyema historia ya
klabu yao.
Amesema kwa mfumo wa kuyaandika mengi mazuri ya klabu ya
Simba alioutumia kuna kila sababu kwa kizazi cha sasa na kijacho kuona mwanzo
wa klabu hiyo mpaka ilivyo sasa na nini matarajio yake.
No comments:
Post a Comment