Mshambuliaji wa Fenerbahce Moussa Sow alifunga goli katika mchezo wa kufuzu dhidi ya Salzburg.
Shauri la zuio la miaka miwili kwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kutokushiriki michuano ya vilabu Ulaya kuendelea ama laa linatarajiwa kufanyika katika ambayo klabu hiyo itakuwa ikicheza dhidi ya Arsenal mchezo wa play-off wa Champions League.
Fenerbahce na Besiktas, ambao walikutwa na hatia ya kupanga matokeo walielekeza kesi yao katika mahakama ya michezo dunia CAS baada ya hukumu ya awali ya zuio la kutokushiriki michuano ya vilabu Ulaya kutolewa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.
Katika taarifa ya CAS kupitia mtandao wake imesema
'Shauri la kesi ya Beşiktaş JK litachukua nafasi Agosti 20 2013 na lile la Fenerbahce SK litasikilizwa Agosti 21 na 22
huko Lausanne.
Mchezo wa marudiano baina yao na Arsenal utafanyika Jumanne ya Agosti 27 siku moja kabla ya maamuzi kutolewa.
Arsene Wenger atakuwa akihitaji kiwango bora siku ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment