KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 19, 2013

Wa-Nigeria wa under U-17 wakutwa na umri mkubwa kuelekea michuano ya kombe la dunia.

Nigeria itawakosa wachezaji wake muhimu katika michuano ya kombe la dunia la wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 mwezi Oktoba baada ya vipimo vya SCAN kuonyesha kuwa walikuwa wamevuka umri. 

Kikosi hicho ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya wachezaji wenye umri huo barani Afrika fainali ambazo zilifanyika nchini Morocco mapema mwaka huu wameonekana kupindukia umri stahili baada ya kufanyiwa kipimo cha SCAN cha MRI( Magnetic Resonance Imaging) mjini Abuja ambacho husaidia kubaini umri halisi kabla ya kuelekea katika michuano ya dunia ambayo itafanyika falme za kiarabu (United Arab Emirates). 

Lakini hata hivyo kocha wa kikosi cha timu ya vijana ya Nigeria "Golden Eaglets" Manu Garba anasema bado atafanikiwa kupata kikosi imara licha ya kuwapoteza wachezaji wake wengi wengi.

Nigeria ilishinda taji la dunia la michuano ya Fifa ya Under-17 mara tatu katika miaka ya 1985, 1993 na 2007 huku mara zote wakikabiliwa na shutuma za umri wa baadhi ya wachezaji wake wanaoliwakilisha taifa hilo.

Bodi ya utawala ya shirikisho la soka dunaini FIFA ilipendekeza kuwepo na kipimo cha MRI kwa lengo la kudhibiti umri katika fainali ya mwaka 2009 mwaka ambao michuano hiyo ilifanyika nchini Nigeria.

Mabingwa wa zamani wa Afrika Ivory Coast, washindi wa pili Nigeria, Tunisia na Morocco wamefuzu kucheza fainali hizo ambazo zitafanyika Falme za Kiarabu kuanzia Oktoba 17 mpaka Novemba 8.
Droo ya michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 26 huko Flame za Kiarabu 'UAE'.

No comments:

Post a Comment