KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, June 2, 2013

LUKAS PODOLSKI AWEKWA SAWA KWENYE RADA YA DORTMUND MAJIRA YA KIANGAZI.

On the radar: Dortmund are interested in signing Arsenal forward Podolski to replace Mario Gotze
On the radar: Dortmund are interested in signing Arsenal forward Podolski to replace Mario Gotze
Borussia Dortmund wako katika mawindo ya kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye alifunga goli katika sekunde ya tisa ya mchezo dhidi ya Ecuador mapema wiki mchezo ambao Ujerumani walichomoza na ushindi wa mabao 4-2 amekuwa ndiye kinara wa mawindo ya mabingwa hao wa soka barani Ulaya katika uhamisho wa majira ya kiangazi.

Meneja Arsene Wenger atakuwa katika vita kubwa ya kumbakisha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 asiende Dortmund, ambayo imempoteza Mario Gotze ambaye anajiunga na Bayern Munich.

Kwasasa Dortmund inataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa Gotze huku taarifa zikisema kuwa naye Robert Lewandowski huenda akaondoka.
No hanging about: Podolski scored two goals, including one in the opening nine seconds, for Germany in a friendly against Ecuador in Florida on Wednesday
Podolski alifunga magoli mawili likiwemo la sekunde ya tisa katika mchezo wa kimataifa wa kirafikia baina ya Ujerumani dhidi ya Ecuador mjini Florida jumatano iliyopita.

Podolksi, alitupia picha akiwa nje ya jengo maarufu la Capitol Hill na ikulu ya Marekani White House hapo jana.
Tourist: Podolski tweeted a picture outside Capitol Hill ahead of Germany's friendly against the USA in Washington DC
Podolski mbele ya jengo la Capitol Hill (juu) na picha ya chini akiwa katika geti la White House pamoja na Miroslav Klose kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya USA mjini Washington DC
Tourist: Podolski tweeted a picture at the gates of the White House with Miroslav Klose ahead of Germany's friendly against the USA in Washington DC

No comments:

Post a Comment