Mabingwa wa
soka nchini Algeria Entente Setif wamefanikiwa kufanya miujiza waliyokuwa
wanaihitaji kuifunga US Bitam ya Gabon katika mchezio wa kusaka nafasi ya
kutinga hatua ya makundi ya michuano ya vilabu ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Setif ilisafiri
kuelekea Gabon ikiwa na kikosi cha wachezaji 14 wakiwemo walinda milango watatu
kwa ajili ya mchezo wao wa mkondom wa pili.
Wenyeji Bitam
walishinda kwa mabao 2-0 hapo jana na kufanya matokeo kusimama 2-2 ambapo
hatimaye wa Algeria hao wakafanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 5-3 ya
magoli ya mikwaju ya penati.
Mlinzi Fares
Abderahmane alifunga goli la penati zuri sana.
Kabla ya
mchezo kocha msaidizi Kheireddine Madoui alikaririwa akisema
"tutaonyesha
miujiza ya kweli kwa kufuzu hatua ya makundi"
Majehi na
kadi nyekundu na za njano zilipelekea Setif kuwakosa walinzi Mohamed Ziti na
Farouk Belkaid (pichani), kiungo Mourad Delhoum na Amir Karaoui pamoja na
washambuliaji Khaled Gourmi na Rachid Naji.
Mabingwa hao
wa ligi ya Algerian maarufu kama Ligue 1 walilazimika kumtumia mlinda mlango Amar
Saadoune kucheza ndani.
Kwingineko Saint
George hii leo inasaka ushindi ili kuwa timu ya kwanza kutoka Ethiopia kufuzu
hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Hii leo
walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Enppi ya Misri wakiwa mbele na ushindi wa
nyumbani wa mabao 2-0 magoli yaliyofungwa na kiungo Shimeles Bekele na mlinzi Abebaw
Butako.
Saint George
walikuwa na matumaini ya kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa kabla ya
matumaini yao kuondolewa na mabingwa wa soka nchini Misri mwezi mjini Cairo
ambapo Zamalek walisonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
Enppi si
pekee kutoka Misri ambao wanapigana kucheza hatua hiyo ya makundi kwani hata
mabingwa wa zamani barani Afrika Ismaily nao wako katika vita ya kutaka
kuidhoofisha CA Bizertin ya Tunisia ambao wako mbele kwa ushindi wa mchezo wa
mkono wa kwanza wa mabao 3-0.
Bizertin inatokea
katika mji wa Bizerte ambao uko kaskazini mwa nchini ya Tunisia.
Neymar: Ronaldo, Kaka & Marcelo walijaribu
kunishawishi nijiunge na Madrid
Neymar amesema
kuwa Cristiano Ronaldo alijaribu kumshawishi ili ajiunge na Real Madrid.
Mbrazilo huyo
alilazimika kuisikiliza zaidi familia yake kabla ya kuamua kujiunga na Barcelona
na anasema kucheza timu moja na nyota kama Lionel Messi kwake ni heshima.
Neymar ametanabaisha
kuwa Cristiano Ronaldo, Kaka na Marcelo walimshawishi sana ili ajiunge na Real
Madrid msimu wa kiangazi kabla ya jaribio lao kushindikana.
Amenukuliwa akisema
"Ronaldo, Kaka,
Marcelo... Lots of people said I should sign for Real," Neymar told Marca.
"But, in the end, I made a decision, which I discussed a lot with my
family, and I'm very happy with the path I've chosen to play in Europe."
No comments:
Post a Comment