Monaco imesainisha mlinzi wa Real Madrid Ricardo Carvalho huku
taarifa zaidi za vyombo vya habari nchini Ufaransa zikisema kuwa klabu hiyo
inamfukuzia mshambuliaji wa Atletico Madrid Radamel Falcao kwa ada ya uhamisho
ya pauni milioni £50.
Mlinzi huyo wa kati wa Chelsea Carvalho mwenye umri wa miaka
35, amekubali kuingia kataba wa mwaka mmoja.
Falcao mwenye umri wa miaka 27 licha ya kuviziwa na Chelsea na
Manchester City, pia anaonekana kutaka kuelekea Monaco.
Klabu hiyo bingwa wa ligi daraja la pili nchini Ufaransa inayo milikiwa na
raia wa Russian Dmitry Rybolovlev, tayari imeshatumia kiasi cha pauni milioni £60
kuwanasa nyota wa Porto Joao Moutinho na James Rodriguez.
Kuhusu Falcao
Born: 10 February
1986
Nationality:
Colombian
Position: Striker
Clubs: River Plate
(2005-2009); Porto (2009-2011) & Atletico Madrid
Atletico stats: 46
league games, 35 goals
Billionaire Rybolovlev amenunua sehemu kubwa ya hisa kwa
mabingwa hao mara saba nchini Ufaransa tangu December mwaka 2011.
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye anashikilia
nafasi ya 119 duniani ya utajiri kwa mujibu wa takwimu za jarida la Forbes inaarifiwa
kuwa anautajiri wa takribani pauni £6bn, akiwa ni mrusi mzalishaji mkubwa zaidi
wa mbolea ya madini ya aina ya potassium.
Rybolovlev amenukuliwa akisema "ana mahaba makubwa na
soka" na anataka kuifanya Monaco kuwa "klabu kubwa nyumbani na Ulaya kwa ujumla
".
Carvalho, ambaye ameichezea mara 75 timu ya taifa ya Ureno
kabla ya kuchana na soka la kimataifa August 2011, amejiunga na klabu hiyo kwa
uhamisho huru.
Gareth Bale huenda
akasikiliza ofa ya Real Madrid, anasema wakala wake
Wakala wa mshambuliaji Gareth Bale anasema huenda mteja wake
akawasikiliza Real Madrid kama watakubaliana na ada iliyotajwa na Tottenham.
Jonathan Barnett ameliambia televisheni ya nchini Hispania
kuwa winga huyo raia wa Wales anaweza kukutana na rais wa Madrid Florentino
Perez.
Akikaririwa wakala huyo amesema "endapo mtu kama Mr
Perez ataonyesha nia kwa Gareth Bale itakuwa ni heshima kubwa na huenda
akasikiliza "
Bale mwenye umri wamiaka 23,bado yuko katika mkataba katika
viunga vya White Hart Lane mpaka 2016 na klabu hiyo ya jijini London huenda
ikaongeza muda zaidi wa mkataba wake.
Barnett anasema kama mchezaji huyo bora mwenye tuzo ya PFA na
tuzo ya waandishi wa habari ataondoka Tottenham, basi huenda ada yake ikawa
zaidi ya ile ambayo Barcelona imelipa kwa ajili ya mshambuliaji nyota wa Brazilian,
Neymar.
Wakati Barcelona wakiwa kimya juu ya kiasi walichotoa kwa Neymar
taarifa za chini ya kapeti zinasema mchezaji huyo amelipiwa pauni milioni £50.
Ametamba kuwa mteja wake ni bora zaidi ya Neymar,
"He's proved
himself in the best league in the world.
"Listen, it's crazy, but whatever Neymar cost, Gareth
Bale is worth more.
"I would hope that any club who wants him, wants him
not because they lost Neymar. I would think he'd have to be their first
choice."
Mark Hughes kumrithi Tony Pulis Stoke City
Meneja wa zamani wa Queens Park Rangers Mark Hughes
anatarajiwa kutangazwa kuwa meneja mpya wa Stoke City mwishoni mwa wiki hii.
Mazungumzo baina ya Hughes na klabu hiyo maarufu (kama Potters)
inaarifiwa kuwa yamekwenda vizuri ambapo Hughes mwenye umri wa miaka 49
inaaminika kuwa katika nafasi ya kwanza ya kupewa kazi hiyo.
Meneja wa Wigan Roberto Martinez na bosi wa zamani wa Sunderland
Martin O'Neill pia wamehusishwa na kutaka kupewa kazi hiyo lakini Hughes ambaye
amekuwa nje ya kazi tangu atimuliwe na QPR mwezi November, ameonekana kuwa
ndiye kinara wa wale wenye maamuzi ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester United,
Barcelona na Chelsea aliaanza kazi ya umeneja akiwa na Wales mwaka 1999 kabla
ya kuondoka na kuwa meneja wa Blackburn mwaka 2004.
Aliondoka Ewood Park miaka minne baadaye na kuelekea katika
klabu ya Manchester City, ambako aliitumikia kwa miezi 18 kabla ya nafasi yake
kuchukuliwa na Roberto Mancini.
Baadaye akapatab mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Fulham kabla
ya kutangazwa kuwa meneja wa QPR mwezi January 2012.
England: Ashley Cole
kuingoza England dhidi ya Ireland uwanja wa Wembley
Mlinzi wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole usiku huu atakuwa
nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachokuwa dimbani dhidi ya
jamhuri Ireland ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya
kutambua heshima yake ya kulitumikia taifa hilo kwa michezo mia moja.
Hapo kabla kulikuwa na mkanganyiko juu ya nani awe kiongozi
uwanjani katika mchezo huo lakini hatimaye Cole akachaguliwa kufuatia kukosekana
kwa Steven Gerrard.
Orodha ya wachezaji waliofikisha jumla ya michezo 100
Peter Shilton
(125)
David Beckham
(115)
Bobby Moore (108)
Bobby Charlton
(106)
Billy Wright (105)
Steven Gerrard
(101)
Ashley Cole (101)
Bosi wa kikosi hicho Roy Hodgson amenukuliwa akisema
"Amekuwa mtumishi bora sit u kwa Arsenal na Chelsea lakini
pia kwa England."
Heshima hiyo kwa Cole inakuja pia baada ya miezi kadhaa
kupita kufuatia kutoa maoni yake kupiatia mtandao wa kijamii wa twitter juu ya
adhabu ya John Terry ambayo yaliyopokelewa kwa vibaya na FA.
Mlinzi huyo alipigwa faini ya pauni £90,000 mwezi October
2012 kwa kuijibu FA juu ya maamuzi yao ya adhabu ya John Terry yaliyohusiana na
ubaguzi wa rangi. Hata hivyo baadaye alifuta maoni hayo na kuomba radhi yeye
mwenyewe kwa mwenyekiti wa FA David Bernstein.
Cole atakuwa anacheza mchezo wa 102 katika kikosi cha England
kitakachokuwa dimba ni Wembley na kuwa mchezaji wa saba kuifikia michezo ya
karne moja aliyoitimiza katika mchezo dhidi ya Brazil mwezi February.
Jamhuri ya Ireland itakuwa inakanyaga Wembley kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1991 ikiwa ni muendelezo wa sherehe za FA kutimiza miaka 150
ambapo pia jumapili watakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Brazil.
Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi dunia
Real Madrid inataka kumfanya Cristiano Ronaldo kuwa ndiye
mchezaji mwenye kulipwa zaidi dunia wakati huu ikiwa katika harakari za kumjengea
mazingira mazuri ya uwepo wake wa baadaye ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo nyota raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 28,
amekuwa akihusishwa na kutaka kuhama na kurejea nchini England katika vilabu
viwili vya ama Manchester United au
kujiunga na Chelsea.
Raia wa Madrid Florentino Perez amenukuliwa na rediao moja
ya Cadena Ser akisema
"Tunaka kuijenga Madrid katika mazingira yanayomzunguka"
"Ningepenga Cristiano kuwa mchezaji anayelipwa zaidi
duniani."
Ronaldo alikuwa mchezaji mwenye thamani kuliko wote duniani
kipindi alipojiunga na Real Madrid akitokea Manchester United kwa ada ya
uhamisho ya pauni milioni £80 June 2009.
Amefunga jumla ya mabao 55 katika jumla ya michezo 55 ya
michuano yote msimu huu lakini pia akifikisha mabao 200 ya kuifungia Real
Madrid mapema mwezi huu tangu ajiunge nayo.
England v Republic of Ireland
Venue: Wembley
Date: 29 May
England itawakosa wachezaji muhimu kwa mara ya kwanza
katika mcheo huo muhimu dhidi ya jamhuri ya Republic ambapo wanakutana kwa mara
ya kwanza tangu mwaka 1995.
Steven Gerrard (bega), Andy Carroll (kiuno), Jack Wilshere (kifundo),
Tom Cleverley (msuli) na Kyle Walker.
Lakini wakati hayo yakiwa hivyo kwa England, wao Los Angeles
Galaxy wamemruhusu mshambuliaji wao hatari Robbie Keane kujinga na kikosi cha
Ireland.
Hapo kabla kulikuwa na hatihati ya Keane kutokujiunga na
kikosi hicho kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mchezo huo uko nje ya ratiba za
michezo ya kimataifa.
England haijawahi kuwa mwenyeji wa Ireland katika dimba la Wembley
tangu zilipokutana kwa mara ya mwisho machi mwaka 1991 katika michezo ya kufuzu
kucheza fainali ya Ulaya.
Mlinzi wa kulia wakati huo Lee Dixon alifunga goli la
wenyeji kabla ya Niall Quinn kuwasawazishia wageni.
England
Goalkeepers: Ben Foster, Joe Hart, Alex McCarthy.
Defenders: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil
Jagielka, Glen Johnson, Phil Jones, Joleon Lescott, Kyle Walker.
Midfielders: Michael Carrick, Frank Lampard, James Milner,
Alex Oxlade-Chamberlain, Jack Rodwell, Theo Walcott.
Forwards: Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Sturridge,
Danny Welbeck.
Republic of Ireland
squad:
Goalkeepers: David Forde, Keiren Westwood, Darren Randolph.
Defenders: John O'Shea, Sean St Ledger, Damien Delaney,
Richard Keogh, Marc Wilson, Seamus Coleman, Stephen Kelly, Darren O'Dea, Paul
McShane.
Midfielders: Glenn Whelan, James McCarthy, Stephen Quinn,
Jeff Hendrick, Aiden McGeady, James McClean, Robbie Brady, David Meyler, Andy
Keogh.
Forwards: Robbie Keane, Shane Long, Connor Sammon, Jon
Walters, Simon Cox, Wes Hoolahan.
Bosi wa soka la Burundi mwanamke Lydia Nsekera kupigiwa kura ya kuingia FIFA
Kiongozi wa chama cha soka cha Burundi FA chief Lydia
Nsekera ni miongoni mwa wagombea wanne wanawake ambao wanawania nafasi ya
ujumbe wa kudumu katika wa kamati ya utendaji ya FIFA yenye kufanya maamuzi(
Fifa's decision-making executive committee).
Fifa inajipanga kuchagua wawakilishi wa muda wote ndani ya
kipindi cha miaka minne katika mkutano utakao fanyika nchini Mauritius, ambao
unaanza kesho alhamisi.
Hii ina maana ya kwamba itakuwa ni kwa mara ya kwanza katika
kipindi cha miaka 109 iliyopita kwa mwanamke kupata haki ya kupiga kura katika
historia ya shirikisho hilo.
Nsekera anasema
"Nafurahi Fifa kumuweka mwanamke katika bodi ya
wakurugenzi, ni jambo chanya hususani kwa wanawake wapenda soka ".
Nsekera, ambaye ameongoza Burundi FA tangu mwaka 2004, anafikiriwa
kushinda katika kinyanganyiro hicho.
Atakuwa akipambana na makamu wa Rais wa zamani wa shirikisho
la soka barani Asia na kiongozi wa soka la kimataifa wa Australia, Maya Dodd, pamoja
na Sonia Bien-Aime wa visiwa vya Turks and Caicos pamoja na Paula Kearns wa New Zealand.
No comments:
Post a Comment