Uganda imemteua Sredojevic 'Micho' Milutin kuwa kocha wa timu
ya taifa.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi
na Bobby Williamson ambaye aliondolewa kazini mwezi April ambapo Micho amesaini
mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.
Micho, ambaye alifukuzwa kazi nchini Rwanda mwezi uliopita
amesema amefurahishwa na kurejea nchini humo ambako ndiko alikoaanzia
kufundisha soka barani Afrika.
Amenukuliwa akisema.
"Ndoto yangu ilianzia 2001 nchini Uganda nilipokuwa na SC
Villa ambapo niliitumiaka kwa miaka mitatu pale. Kwa miaka tisa iliyopita
nilikuwa nikifundisha soka nchini Ethiopia, Sudan, South Africa, Tanzania na
Rwanda. Sasa nimerejea katika nyumba yangu ya soka.
"Nimefurahia na nitafanya kila niwezalo kufikia malengo
ya kuboresha timu.
Rais wa chama cha soka nchini Uganda , Lawrence Mulindwa, amesema
jumla ya watu 37 waliomba kazi hiyo na kwamba wanamuhakikishia Micho kwamba watampa ushirikiano.
Wasaidizi wa zamani wa Cranes Sam Timbe na Kefa Kisala pia
wametajwa kumsaidia Micho's assistant coaches, huku Fred Kajoba akisalia katika
nafasi ya kocha wa makipa.
Sredojevic alianza kuifundisha Rwanda mwezi November 2011, alipochukua
nafasi ya Sellas Tetteh wa Ghana.
Mafanikio makubwa akiwa na Amavubi ni pale alipomaliza
katika nafasi ya pili katika michuano ya Cecafa Senior Challenge mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment