KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 26, 2012

KOCHA WA RWANDA ERICK NSHIMIYIMANA ANASEMA KILIMANJARO STARS HAIKAMATIKI AITABIRIA UBINGWA.

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda(Amavubi) Erick Nshimiyimana amesema ameiangalia kwa makini timu ya taifa ya Tanzania Bara(Kilimanjaro Stars) na kutamka maneno haya "Hii haikamatiki".
 
Nshimiyimana alitoa kauli hiyo nzito baada ya kuishuhudia Kilimanjaro Stars ikiifunga Sudan mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano ya chalenji uliopigwa hapo jana kwenye uwanja Namboole jijini Kampala.
Amekaririwa akimuuliza kwa mshangao mwandishi wa habari hii,
"Hivi huyu kocha ana muda gani?(mwandishi wa habari hii alimjibu kuwa hata mwaka hajafikisha tangu alipokabidhiwa timu ndipo alipoendelea kusema.
"Hii timu imebadilika sana kama itaendelea kucheza hivi hakuna ubishi kwamba itafika mbali na huenda ikachukua hata ubingwa,".alisema Nshimiyimana.

Nshimiyimana ambaye pia ni kocha wa timu ya APR  ya Rwanda amesema, Kilimanjaro Stars imekamilika kila idara kuanzia ufundi hadi fiziki ya wachezaji.
 
"Nimewaangalia kwenye fiziki na hata mbinu wako vizuri na hata wanapotengeneza mashambulizi unaona kabisa yamepangiliwa,"
 
Kilimanjaro Stars hapo jana walianza vema kampeni yake ya kuwania taji la Chalenji baada ya mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na John Raphael Bocco kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudini mchezo ambao ulikuwa ni wa pili wa kundi la B wa michuano ya kombe la Chalenji mchezo ambo ulifanyika katika uwanja wa Namboole. 

No comments:

Post a Comment