KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 30, 2013

Kocha akataa kazi kutokana na ghasia za nchini Libya.


Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tunisia Nabil Maaloul amegoma kuchukua nafasi ya kukinoa kikosi cha Ahly Tripoli kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo iliyo kazkazini mwa Afrika.

Maaloul aliondoka katika nafasi yake ya kuifundisha Tunisia maarufu kama 'Carthage Eagles' baada ya kushindwa kufuzu kuingia katika hatua ya mtoano ya kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia kabla ya kupata nafasi hiyo kwa gharama za Cape Verde ambayo ilimchezesha mchezaji asiyeruhiswa kuchezea nchi hiyo.

Vyombo vya habari nchini Tunisia vimearifu kuwa Nabil amekataa kufanya kazi na Al Ahly Tripoli kutokana na hali ya usalama.

Kocha mkuu wa Al Ahly Tripoli Hossam El Badry mapema alitangazaa kuondoka na kuwa hatarejea ndani ya kikosi chake baada ya kutokea matukio ya kutupiana risasi.

Sasi Buown mwenyekiti wa Al Ahly Tripoli alitembelea El Badry mjini Cairo kujaribu kumshawishi kurejea lakini inavyoonekana ameshindwa.
Al Ahly Tripoli iko katika nafasi ya pili katika kundi A la ligi ya Libya ikiwa na alama saba baada ya kushinda michezo miwili na kwenda sare mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment