KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 4, 2013

NIGERIA WATOTO WANAKARIBIA KUTWAA KOMBE LA DUNIA.

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Alhaji Issa Hayatou, hii leo ametembelea kambi ya timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Nigeria maarufu kama Golden Eaglets wakiwa katika maandalizi ya kuweka rekodi ya kutwaa taji la dunia la nne la michuano ya kombe la dunia fainali zake zikifanyika huko Falme za kiarabu.
Hayatou, akiwa ameongozana na makamu wake Almamy Kabele Camara, na mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya FIFA Mohamed Raouraoua, Wamekipongeza kikisi hicho cha vijana wa Nigeria baada ya kufanya vizuri katika mchezo wao uliopita wa hatua ya robo fainali dhidi ya Uruguay uliopigwa Jumamosi.
Amenukuliwa akisema
“Mmeonyesha saka la hali ya juu katika michuano hii na sijawahi kuona timu ya kutoka Afrika ikicheza soka safi kiasi kile . Sishangazwi na ukubwa wa soka lenu kwani niliwaona katika michezo ya vijana ya Afrika CAN dhidi ya Morocco na nilivutiwa sana.

Rais wa soka la Nigeria, Alhaji Aminu Maigari, ambaye alimpokea Rais CAF wakati wa ziara hiyo amepongeza ziara ya hiyo na kumuhakikishia bosi huyo wa soka Afrika kuwa katika nusu fainali dhidi ya Sweden timu hiyo itafanya vizuri na kwamba ziara yake hiyo nin chachu ya ushindi ndani ya uwanja wa Rashid mjini Dubai.

No comments:

Post a Comment