| Pambano la masumbwi ya kulipwa baina ya mabondia wa Sukkasem Kietyongyuth wa Thailand na Francis Miyeyusho( Pichani juu) na Fransic Cheka wa Tanzania dhidi ya Gavad
Zohrehvand wa Iran( Pichani chini) limeahirishwa mpaka Jumamosi ijayo. Taarifa zinasema kuwa kuahirishwa huko kumetokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kujaza maji katika ukumbi wa PTA ambao ungetumika kwa ajili ya mapambano hayo. Taarifa hizi zimethibtishwa na Rais wa PST Immanuel Mlundwa ambaye shirikisho la lake lilikuwa likishirikiana na mwaandaaji wa mapambano hayo Promota Musa Kova. |
|
No comments:
Post a Comment