Pages - Menu

Wednesday, July 23, 2014

Azam fc na Ruvu Shooting kupima ubavu uwanja wa Chamazi

Maafande wa jeshi la kujenga taifa kutoka mkoani Pwani, Ruvu Shooting kesho watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania bara Azam FC katika uwanja wa Azam Coplex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema mchezop huo wa kesho wanaamini utawapa taswira ya maandalizi yao ambayo walianza kuyafanya tangu mwanzoni mwa mwezi June, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi mbao utaanza kutimua vumbi lake Septemba 20.

No comments:

Post a Comment