Utakuwa ni mpambano wa kufa na kupona, katika siku ya mwisho ya msimu
katika ligi kuu ya soka Uhispania, wakati Barcelona watakapowakaribisha
Atletico Madrid uwanjani Camp Nou.
Mechi hiyo ndiyo itakayoamua mshindi wa msimu huu wa taji la ligi kuu ya
soka Uhispania, baada ya timu zote mbili kwenda sare katika michezo yao ya mwisho.
Ni wazi kuwa Real Madrid hawako tena katika kinyang'anyiro
hicho, baada ya kuduwazwa na Celta Vigo kwa kurambishwa magoli mawili
bila jawabu.
Atletico walitoka sare ya goli moja kwa moja na Malaga, wakati Elche
wakiwateka miamba Barcelona kwa kutofungana goli lolote.
Atletico sasa
watahitaji tu sare watakapokutana na Barca kesho, lakini kama Barca watapata
alama tatu, basi wataweza kulichukua taji hilo kwa sababu watakuwa na alama 89 kila mmoja, ila tu Barca watatawazwa mabingwa kwa sababu ya
rekodi ya kuzilinganisha timu hizo mbili ambayo hutumiwa kuamua mshindi.
No comments:
Post a Comment