KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 23, 2012

SIMBA NA MATHARE JUMAPILI,OKWI KUJIUNGA NA SIMBA AUGUST 28

 

 
Mabingwa wa kandanda wa nchini Tanzania Simba imeialika klabu ya soka ya Mathare United ya Kenya kucheza mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika katika uwanja wa taifa jumapili.
Simba wanatarajia kucheza mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam kwa tarehe ambayo bado haijatajwa na shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na kamati ya ligi  na vilabu.
Akiongea na Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema ni mechi nzuri kwa mwalimu kuona kikosi chake ambacho kinaendelea na mazoezi mjini Arusha .
Amesema Mathare ni timu nzuri ambayo iko katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu ya Kenya ikiwa na points 19.
 Katika hatua nyingine Ezekile Kamwaga amewashusha pumzi mashabiki wa klabu hiyo juu ya mshambulaiji Emmanuel Okwi ambaye katika kipindi kirefu bado ameshindwa kuangana na kikosi hicho licha ya kutambulishwa katika takasha la Simba maarufu kama Simba Day ambalo lilifanyika August 8 uwanja wa taifa.
 
Kamwaga amesema Okwi atajiunga rasmi na Simba mara baada ya mchezo wa kimataifa kati ya Kenya na Botswana mchezo ambao umepangwa kufanyika August 26 jijini Gaborone.
Amesema Okwi alikuwa bado anasumbuliwa na malaria hivyo alikuwa bado anaendelea na matibu nyumbani kwao Kenya na kwamba kwasasa anaendelea vizuri lakini yuko kambini na timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars na anatazamiwa kujiunga na kambi ya Simba siku mbili baada ya mchezo huo.
 

No comments:

Post a Comment