
Mabingwa wa
kandanda wa nchini Tanzania Simba imeialika klabu ya soka ya Mathare United ya
Kenya kucheza mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika katika uwanja wa taifa jumapili.
Simba wanatarajia
kucheza mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam kwa tarehe ambayo bado haijatajwa
na shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na kamati ya ligi na vilabu.
Akiongea na
Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema ni mechi nzuri kwa
mwalimu kuona kikosi chake ambacho kinaendelea na mazoezi mjini Arusha .
Amesema
Mathare ni timu nzuri ambayo iko katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi
kuu ya Kenya ikiwa na points 19.
Katika hatua nyingine Ezekile Kamwaga
amewashusha pumzi mashabiki wa klabu hiyo juu ya mshambulaiji Emmanuel Okwi
ambaye katika kipindi kirefu bado ameshindwa kuangana na kikosi hicho licha ya
kutambulishwa katika takasha la Simba maarufu kama Simba Day ambalo lilifanyika
August 8 uwanja wa taifa.
Kamwaga
amesema Okwi atajiunga rasmi na Simba mara baada ya mchezo wa kimataifa kati ya
Kenya na Botswana mchezo ambao umepangwa kufanyika August 26 jijini Gaborone.
Amesema Okwi
alikuwa bado anasumbuliwa na malaria hivyo alikuwa bado anaendelea na matibu nyumbani
kwao Kenya na kwamba kwasasa anaendelea vizuri lakini yuko kambini na timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars na anatazamiwa kujiunga na kambi ya Simba siku mbili baada ya mchezo huo.

No comments:
Post a Comment