Klabu ya
simba ya jijini Dar es Salaam imewasilisha barua yake shirikisho la soka nchini
TFF la kutaka kuondolewa kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya katiba ,sheria na
hadhi ya wachezaji katika kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wawili
Kelvin Patrick Yondani na Mbuyi Twite kuhusu .
Simba katika
barua hiyo imewataja baadhi ya wajumbe hao kuwa ni pamoja na Iman Madega , Alex
Mgongolwa na Lyod Nchunga ambao ni wanachama na wamewahi kuwa viongozi wa Yanga
kwa nyakati tofauti.
Akiongea na
Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kimsingi huwezi
kupeleka kesi ya namna hiyo katika kamati ambayo ina wajumbe wengi ambao
wanamapenzi na klabu ambayo ndiyo inayoshitakiwa ukategemea haki kutendeka.
Amesema
Madega na Nchunga wameshawahi kuwa kwenye nafasi ya mwenyekiti ya Yanga wakati
ambapo Alex Mgongolwa inaaminika kuwa ni mwanachama mkereketwa wa klabu
hiyo.
Kamati ya
katiba ,sheria na hadhi ya wachezaji inaongozwa na mwenyekiti Alex Mgongolwa, makamu
mwenyekiti Husein Mwamba na wajumbe Imani Madega,Venance Mwamoto,Omari Gumbo ,Ismail
Aden Rage na Lloyd Nchunga.
Suala la kujiuliza ni je vipi kuhusu Aden Rage na Omari Gumbo ambao nao ni wanachama wa Simba?
Kwasasa Rage ndio Mwenyekiti na Omari Gumbo kabla ya Uongozi wa sasa alikuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo.
BOFYA HAPA

No comments:
Post a Comment