Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki
(IOC) inamsubiri mwendesha baiskeli wa Marekani aliyepatikana na hatia
ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini Lance Armstrong arejeshe
medali ya shaba aliyoshinda kwenye mashindano ya Olimpiki ya mjini Sydney
mwaka 2000, kwa mujibu wa mkuu wa tume ya sheria ya IOC.
Kamati hiyo ya IOC ilimuandikia Armstrong mnamo
mwezi Januari mwaka huu kumtaka arejeshe medali hio ingawa Bach alikiri
kwamba mwendesha baiskeli huyo alikiri makosa yake lililobaki ni
kutimiza ahadi yake ya kukabidhi medali.
Bach
ameongezea kusema kuwa walitangaza matokeo hayo kua yasiyo sihi na
nafasi hio kumkabidhi Abraham Olano wa Uhispania aliyemaliza wa nne.
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ilichelewesha
kumuadhibu Lance Armstrong hadi shirika linalotawala mchezo wa
mashindano ya baiskeli (international Cycling Union -UCI)
lilipoidhinisha hatua ya Armstrong kuchukuliwa hatua kufuatia majuma
matatu ambapo mtuhumiwa alikua na fursa ya kukata rufaa.
Kilichofuata ni hatua ya kumnyang'anya Armstrong
medali zote saba alizoshinda kwenye mashindano ya mbio za Ufaransa
maarufu kama Tour de France na kupigwa marufuku daima asishiriki
mashindano mengine maishani mwake.
Haya yalifuatia ushahidi wa taasisi ya Marekani inayopambana na matumizi ya dawa za kuongezea nguvu mwilini
(USADA).
Baada ya ubishi mkali marafiki wa Armstrong
walitoa ushahidi uliombana yeye na baadhi ya washirika wake kua kweli
alitumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
No comments:
Post a Comment