KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 9, 2013

Mbio za rungu la Commonwealth

Malkia wa Uingereza ameanzisha rasmi mbio za kupokezana rungu la michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika mjini Glasgow Scotland mwaka 2014.
Rungu hiyo ina risala aliyoiandika kwa mkono Malkia kwa Jumuiya ya Madola itakayosafirishwa katika mataifa na maeneo yote 70 yatakayoshiriki katika michezo hiyo katika kipindi cha siku 288 zijazo.
Rungu hilo litasafirishwa kwanza hadi Scotland mnamo siku ya Alkhamisi kabla ya kuelekea India kwa kituo chake cha kwanza cha kimataifa Octoba 11.
Safari ya rungu hilo itamalizika wakati wa sherehe za ufunguzi za michezo hiyo Julai 2014, ambapo Malkia ataisoma risala iliyomo ndani yake.
Katika sherehe za uzinduzi ziliofanyika katika kasri ya Malkia mjini London, rais wa Shirikisho la michezo ya Commonwealth , Prince Imran wa Malaysia, amesema mbio za rungu hilo lina ujumbe mzito wenye maana.
"mbio za kupokezana rungu hilo zinawaunganisha raia billioni 2 wa Commonwealth katika kusherehekea michezo,kabila tofauti na amani na kudumisha urafiki na uhusiano wetu" alisema Imran
Baada ya hotuba Malkia alitumbukiza waraka wenye risala yake ndani ya rungu hilo na kisha kufungwa kwa safari yake ya kilometa 190,000 kupitia mabara ya Asia, Oceania, Afrika, Amerika za Kaskazini na Kusini na Caribbean.
Wa kwanza kukimbiza rungu hilo alikua Alan Wells,mwanariadha wa mbio fupi wa Scotland aliyeshinda medalli ya dhahabu katika mbio za mita 100 za Olimpiki ya 1980 mjini Moscow.

No comments:

Post a Comment