KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 8, 2013

MFUPA ULIWASHINDA CAMEROON WACHUKULIWA NA LIBYA.

Shirikisho la soka  nchini Libya LFF limethibitisha kumuajiri kocha wa timu ya taifa kutoka nchini Hispania Javier Clemente.
Kocha huyo wa zamani wa Hispania anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdelhafidh al-Rabich, ambaye alijiuzulu baada ya Libya kushindwa kufuzu kwa hatua ya mwisho ya kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia 2014.
Taarifa zinasema kuwa kocha huyo mpya ameingia mkataba wa miaka miwili muda ambao hautajumuisha mwaka ambao watakuwa wakiaandaa michuano ya mataifa ya Afrika 2017.
Akiongea amesema
"Nimepewa mpango wa kutengeneza mazingira ya kuwezesha kujenga timu nzuri" 
"Bado sielewi kiwango cha soka la Libya, nitachukuwa muda kujifunza na kurekebisha fikra za watu na filosofia ya mchezo hapa."
Kzi kubwa mbele yake ni kuiongoza kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Morocco mwaka 2015 wakati ambapo michezo ya kufuzu ikitarajiwa kuanza mwakani mwezi Septemba.
Clemente amezifundisha Marseille ya Ufaransa na Espanyol ya hispania kabla ya kuifundisha Athletic Bilbao.
Alikuwa kocha wa Cameroon kwa mwaka kabla ya kufungishwa virago baada ya kushindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012. 

No comments:

Post a Comment