KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 8, 2013

Ghana wataka mchezo wao wa marudiano dhidi ya Misri kuchezwa nje ya nchi hiyo katika uwanja huru.

Chama cha soka nchini Ghana GFA kimeliomba shirikisho la soka duniani Fifa kuuondoa mchezo wa kuwania tiketi ya kombe la dunia ambao utakuwa ni wa mkondo wa pili kuondolewa nchini Misri na kupelekwa katika uwanja huru.
Kufuatia watu kadhaa kuuwawa mwishoni mwa juma katika ghasia za nchini Misri hususani katika jiji la Cairo, GFA imesema kuwa hiyo ni kwa mujibu wa mustakabali wa kiusalama.
Mchezo baina yao jijini Cairo unatarajiwa kufanyika Jumanne ya Novemba 19.
GFA kupitia mtandao wake wameandika 
"Maombi yetu yamezingatia hali ya usalama nchini Misri, vurugu zinaonyesha kuwa hakuana dalili ya kudhibitiwa
"The violence has shown no sign of abating.
"Tunahusika na mambo ya usalama wa msafara wetu na wasimamizi wa mchezo endapo mchezo huo uatachezwa Misri.

No comments:

Post a Comment